Antelmi wa Belley
Antelmi wa Belley, O.Cart. (Chignin, Chambery, Ufaransa, 1107 - Belley, Ufaransa, 26 Juni 1178) alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 1163 hadi kifo kifo chake[1].
Baada ya kuingia ukleri, alipofika umri wa miaka 30 aliingia katika monasteri ya Wakartusi huko Chartreux na miaka 2 baadaye akawa priori bora kwa miaka 22, isipokuwa katikati alikwenda kuishi upwekeni kwa miaka michache.
Alipata kuwa mkuu wa kwanza wa shirika hilo lote la Mt. Bruno.
Alijitahidi kurekebisha maadili ya jimbo lake.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Juni[2].
Tazama pia[hariri | hariri chanzo]
- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints. 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993. ISBN 0-14-051312-4.
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- Catholic online article on St. Anthelm, retrieved 23 May 2007
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |