Aneth David
Aneth Bella David ni mwanasayansi, mtafiti katika masuala ya bioteknolojia na mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam[1]. Utaalamu wake unajumisha matumizi ya zana za kibioteknolojia kwa maendeleo endelevu katika kilimo na afya. Anafundisha na kufanya utafiti juu ya viumbe hai, ukinzani wa antimicrobial na teknolojia ya viumbe vidogo.[2]
Pia ni mwanzilishi mwenza wa shirika la Tanzania Human Genetics Organization (THGO), mpango unaolenga kupanua utafiti wa binadamu nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla[3].
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Aneth alihitimu elimu yake ya sekondari katika Shule ya Sekondari Mawenzi (2007) mkoani Kilimanjaro, elimu ya upili katika shule ya upili Majengo (2010) Majengo, mjini Moshi, Shahada ya awali ya Biolojia ya Molekuli na Bioteknolojia katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (2013), shahada ya uzamili ya Bioteknolojia (2016) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na PhD (Udaktari wa Falsafa) katika masuala ya Biolojia katika Chuo Kikuu cha Uswidi cha Sayansi ya Kilimo mnamo mwaka 2022[4][5].
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]Aneth ametambuliwa kwa nafasi yake katika utetezi wa sayansi kupitia tuzo mbalimbali zikiwemo tuzo ya ubalozi wa Next Einstein Forum (NEF) (2015), Malkia wa Nguvu (2018), Tanzanian sheroes (2018) na NEF women in STEM (2022)
Machapisho
[hariri | hariri chanzo]Aneth ametoa machapisho mbalimbali kama vile[6][7]
- Long-term maize-Desmodium intercropping shifts structure and composition of soil microbiome with stronger impact on fungal communities (2021)
- Genetic, epigenetic and phenotypic diversity of four Bacillus velezensis strains used for plant protection or as probiotics (2019)
- Rare diseases in Tanzania: a national “Call for Action” to address policy and urgent needs of individuals with rare diseases (2022)
- A Baseline evaluation of bioinformatics capacity in Tanzania reveals areas for training (2021)
- Changing scientific meetings for the better (2021)
- A Baseline evaluation of bioinformatics capacity in Tanzania reveals areas for training (2021)
- Revisiting push-pull technology: Below and aboveground mechanisms for ecosystem services (2022)
- Valorization of palm oil wastes into oyster mushrooms (Pleurotus HK-37) and biogas production (2023)
- The status and challenges of preprint adoption in Africa (2024)
- Baseline Evaluation of Bioinformatics Capacity in Tanzania (2020)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "University of Dar es Salaam - College Of Natural And Applied Sciences | Staff List". www.udsm.ac.tz. Iliwekwa mnamo 2024-08-30.
- ↑ Valine Moraa (2024-07-08). "Dr Aneth David, Tanzania". BioInnovate Africa (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-08-30.
- ↑ "Dr. Aneth David – Tanzania Human Genetics Organization" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-08-30.
- ↑ "University of Dar es Salaam - College Of Natural And Applied Sciences | Staff List". www.udsm.ac.tz. Iliwekwa mnamo 2024-08-31.
- ↑ "Aneth Bella David". SLU.SE (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-08-31.
- ↑ "Aneth Bella David". scholar.google.com. Iliwekwa mnamo 2024-08-31.
- ↑ "University of Dar es Salaam - College Of Natural And Applied Sciences | Staff List". www.udsm.ac.tz. Iliwekwa mnamo 2024-08-31.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Aneth David kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |