Amr Darrag

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ahmed Amr Darrag (alizaliwa Oktoba mwaka 1958) ndiye mwanzilishi na mwenyekiti wa Taasisi ya Mafunzo ya Misri (EIS). EIS ni taasisi ya wataalam yenye makao yake mjini Istanbul, Uturuki. Yeye ni mhandisi na mwanasiasa wa Misri, ambaye alihudumu kwa muda mfupi kama waziri wa mipango na ushirikiano wa kimataifa wa Misri kuanzia tarehe 7 Mei hadi 4 Julai 2013 chini ya serikali iliyoongozwa na Chama cha Freedom and Justice Party.

Maisha ya mapema na elimu[hariri | hariri chanzo]

Darrag alizaliwa Oktoba 1958. Ana shahada ya kwanza katika uhandisi wa ujenzi na shahada ya uzamili ya mechanics ya udongo na misingi aliyo ipata kutoka Chuo Kikuu cha Cairo mnamo 1980 na 1984. [1] Alipata Shahada ya Uzamivu katika mechanics ya udongo na misingi kutoka Chuo Kikuu cha Purdue mwaka wa 1987. [2]

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Darrag ameoa na ana watoto watatu wa kike.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Nancy Messieh (7 May 2013). Profiling Egypt's New Ministers. Atlantic Council. Jalada kutoka ya awali juu ya 7 June 2013. Iliwekwa mnamo 17 June 2013.
  2. Amr Darrag. World Economy Forum. Iliwekwa mnamo 18 June 2013.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Amr Darrag kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.