Nenda kwa yaliyomo

Amoni, Zeno na wenzao

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Amoni, Zenoni na wenzao)

Amoni, Zeno na wenzao Tolomayo, Ingene na Theofilo (walifia dini Aleksandria, Misri, 249 hivi) wakati wa dhuluma ya kaisari Decius.

Theofilo alikuwa mzee, wengine wanne askari; wakiwa mahakamani wakati Mkristo mwenzao alipokuwa anateswa ili aache imani, walikuwa wanamtia moyo asizidi kuyumba kutokana na maumivu makali. Hapo umati uliwapigia kelele, nao wakajitosa katikati kujitangaza Wakristo wakauawa mara moja[1].

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 1 Juni[2][3].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.