Nenda kwa yaliyomo

Amoni, Zeno na wenzao

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Amoni, Zeno na wenzao Tolomayo, Ingene na Theofilo (walifia dini Aleksandria, Misri, 249 hivi) wakati wa dhuluma ya kaisari Decius.

Habari zao zinapatikana katika Historia ya Kanisa iliyoandikwa na Eusebi wa Kaisarea akiripoti barua ya Dionisi wa Aleksandria kwa Fabio wa Antiokia [1].

Theofilo alikuwa mzee, wengine wanne askari; wakiwa mahakamani wakati Mkristo mwenzao alipokuwa anateswa ili aache imani, walikuwa wanamtia moyo asizidi kuyumba kutokana na maumivu makali. Hapo umati uliwapigia kelele, nao wakajitosa katikati kujitangaza Wakristo wakauawa mara moja [1][2][3].

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama watakatifu wafiadini[4][2][5] .

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 1 Juni[6][7][8].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. 1 2 Storia ecclesiastica, Libro VI, capitolo 41, 22. Tafsiri ya Kiingereza: Philip Schaff, Eusebius Pamphilius: Church History, Life of Constantine, Oration in Praise of Constantine, Christian Classics Ethereal Library, nº 22.
  2. 1 2 Moreschini, Bibliotheca Sanctorum, I, p. 1012
  3. https://www.santiebeati.it/dettaglio/55510
  4. (Kilatini) Jacques Dubois, Le martyrologe d'Usuard. Texte et commentaire, (Subsidia hagiographica, N°40), Bruxelles, Société des bollandistes, 1965, p. 362.
  5. https://www.sursumcorda.cloud/downloads/Martirologio-Romano.pdf Martirologio romano pubblicato per ordine del Sommo Pontefice Gregorio XIII, riveduto per autorità di Urbano VIII e Clemente X, aumentato e corretto nel 1749 da Benedetto XIV, quarta edizione italiana, Libreria editrice vaticana, 1955, pp. 328-329
  6. Martyrologium Romanum
  7. De sanctis martyribus Ammone, Zenone, Ptolomaeo, Ingene et Theophilo militibus, Acta Sanctorum Junii, vol. I, 1867, pp. 31-32.
  8. https://catholicsaints.info/martyrs-of-alexandria-1-june/

Marejeo ya Kiswahili

[hariri | hariri chanzo]
  • John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 456-457
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 395

Marejeo ya lugha nyingine

[hariri | hariri chanzo]
  • Augusto Moreschini, Ammone, Zenone, Tolomeo, Ingene e Teofilo, soldati, santi, martiri di Alessandria, Bibliotheca Sanctorum, I, pp. 1012-1013.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.