Nenda kwa yaliyomo

Alyson Hannigan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alyson Hannigan

Alyson Hannigan mnamo mwezi wa Mei 2015
Amezaliwa Alyson Lee Hannigan
24 Machi 1974 (1974-03-24) (umri 50)
Washington, D.C., Marekani
Jina lingine Alyson Denisof
Kazi yake Mwigizaji
Miaka ya kazi 1986–hadi sasa
Ndoa Alexis Denisof (tangu 2003- hadi sasa)
Watoto 2

Alyson Lee Hannigan (amezaliwa tar. 24 Machi, 1974) ni mwigizaji wa filamu na tamthilia kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa kucheza uhusika wa Willow Rosenberg kwenye mfululizo wa kipindi cha Televisheni cha Buffy the Vampire Slayer (1997–2003), Lily Aldrin kwenye ucheshi wa How I Met Your Mother kupitia TV ya CBS (2005–hadi sasa) na Michelle Flaherty katika mfululizo halisi wa filamu za American Pie (1999; 2001; 2003; 2012).[1]

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Hannigan alizaliwa mjini Washington, D.C. ni mtoto pekee wa Bi. Emilie (Posner) Haas, wakala wa masuala ya ardhi na viwanda, na Bwana Al Hannigan, dereva wa magari makubwa ya safari.[2] Baba'ke ni Mwamerika mwenye asili ya Ireland na mama'ke ni Myahudi.[3][4] Wazazi walitalikiana wakati ana umri wa miaka miwili tu na muda mwingi alilelewa na mama'ke tu huko mjini Atlanta, Georgia.[5]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

1978 – 1996[hariri | hariri chanzo]

Akiwa na umri wa miaka minne, Hannigan akaanza kuonekana katika matangazo.[6] Alihamia mjini Hollywood akiwa na umri wa miaka 11.[7] Akiwa anaishi na mama'ke na baadaye kuhitimu katika shule ya North Hollywood High School, baadaye akajiunga na Chuo Kikuu cha "California State", Northridge ambapo alipata shahada ya saikolojia.

Uhusika mkubwa kabisa wa kwanza wa Hannigan wa kwenye filamu ya My Stepmother Is an Alien,[1] toleo la ubunifu wa kisayansi ambalo pia linavichekesho ndani yake mnamo 1988; mmoja kati ya washirika wenza katika filamu hiyo alikuwepo mwigizaji Seth Green, ambaye baadaye aliungana nae kama muhusika wa kawaida katika tamthilia ya Buffy akiwa kama bwana wake. Kisha mwaka wa 1989, uhusika wake wa kawaida wa kwanza kwenye mfululizo wa TV ulikuja pale aliposhirikishwa kwenye ucheshi mfupi wa Free Spirit.

Akiwa msichana, Hannigan aliwatunza watoto wa Bob Saget, ambaye baadaye alikuja kuhadithia katika mfululizo wake wa TV , How I Met Your Mother.[8]

1997 – hadi sasa[hariri | hariri chanzo]

Mwaka wa 1997, Hannigan alichaguliwa kucheza uhusika wa Willow Rosenberg, rafiki wa karibu wa Buffy Summers, katika mfululizo wa televisheni wa Buffy the Vampire Slayer.[9] Kipindi hicho kilipata mafanikio makubwa mno, na Hannigan akapata kutambulika vya kutosha, hatimaye kuonenakana katika nyusika maarufu kadha wa kadha ambazo zililenga hasa watazamaji vijana, ikuwa ni pamoja na American Pie, American Pie 2, Boys and Girls na American Wedding.[1] Pia alipata kuonekana kiduchu kwenye mfululizo unaotokana na hadithi ya Buffy, Angel, akitumia tena uhusika wake uleule wa Willow katika vipengele kadhaa (ikiwa ni pamoja na "Orpheus," wakati wa msimu wa nne wa Angel na msimu wa saba wa Buffy), lakini hakuna tena baada ya Buffy kumaliza kutayarishwa kwake.

Mwaka wa 2012, Hannigan ameurudia tena uhusika wake wa Michelle kwenye American Reunion.[10]

akiwa na mumewe Alexis Denisof

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Hannigan ameolewa na mwigizaji mwenzake wa katika tamthilia ya Buffy the Vampire Slayer Alexis Denisof katika hoteli ya Two Bunch Palms Resort huko mjini Desert Hot Springs, California, mnamo tar. 11 Oktoba, 2003. Wawili hao wana watoto wawili wa kike, Satyana Marie Denisof, amezaliwa mnamo tar. 24 Machi, 2009,[11] na Keeva Jane Denisof, amezaliwa mnamo tar. 23 Mei, 2012.[12] Hannigan ni mama mlezi wa mtoto wa kiume wa Joss Whedon, Arden, na mume wake, Alexis Denisof, ni baba mlezi wake.[13]

Filmografia[hariri | hariri chanzo]

Filamu
Mwaka Jina Uhusika Maelezo
1986 Impure Thoughts Patty Stubbs Kama Alyson Hannigan
1988 My Stepmother Is an Alien Jessie Mills
1991 Switched at Birth Gina Twigg, Umri 13–16 Filamu ya TV
1995 The Stranger Beside Me Dana Filamu ya TV
1996 Case for Life Iris Filamu ya TV
1996 For My Daughter's Honor Kelly Filamu ya TV
1998 Dead Man on Campus Lucy
1999 Hayley Wagner, Star Jenna Jakes Filamu ya TV
1999 American Pie Michelle Flaherty
2000 Boys and Girls Betty
2001 American Pie 2 Michelle Flaherty
2001 Beyond the City Limits Lexi
2003 American Wedding Michelle Flaherty
2004 Americana Andrea Filamu ya TV
2005 In the Game Haijulikani Mfululizo wa TV
2006 Date Movie Julia Jones
2011 Love, Wedding, Marriage Courtney Amecheza na mume wa maisha ya kweli Alexis Denisof
2012 American Reunion Michelle Flaherty-Levenstein
Televisheni
Mwaka Jina Uhusika Maelezo
1989–1990 Free Spirit Jessie Harper Muhusika mkuu; vipengele 14
1990 Roseanne Jan Kipengele: "Like, a New Job"
1993 Almost Home Samantha Kipengele: "The Dance"
Episode: "Hot Ticket"
1994 Touched by an Angel Cassie Peters Kipengele: "Cassie's Choice"
1996 Picket Fences Peggy Patterson Kipengele: "To Forgive Is Devine"
1996 Friends for Life Emma Daniels Unaired TV Pilot
1997–2003 Buffy the Vampire Slayer Willow Rosenberg Muhusika Mkuu; vipengele 144
1999–2000 100 Deeds for Eddie McDowd Gigi Kipengele: "Dogs Day Out"
Episode: "The Return of Gigi"
2000 Wild Thornberrys Gerda Kipengele: "Every Little Bit Alps"
2001–2003 Angel Willow Rosenberg Kipengele: "Disharmony"
Kipengele: "There's No Place Like Plrtz Glrb"
Episode: "Orpheus"
2004 That '70s Show Suzy Simpson Kipengele: "Sally Simpson"
Episode: "Won't Get Fooled Again"
2004 King of the Hill Stacey Gibson Kipengele: "Talking Shop"
2005 Veronica Mars Trina Echolls Kipengele: "Ruskie Business"
Kipengele: "Hot Dogs"
Kipengele: "My Mother, the Fiend"
2005–hadi sasa How I Met Your Mother Lily Aldrin Uhusika Mkuu
2009 Goode Family Michelle Kipengele: "Graffiti in Greenville"
2011 The Simpsons Melody Msimu wa 22: Kipengele 11: "Flaming Moe"
2011 American Dad Chelsea Msimu wa 7: Kipengele cha 5: "Virtual In-Stanity"

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. 1.0 1.1 1.2 "How I Met Your Mother Cast: Alyson Hannigan". CBS. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-05-31. Iliwekwa mnamo 2012-06-12.
 2. "Film Reference Alyson Hannigan Bio". Filmreference.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-02-10. Iliwekwa mnamo 2010-03-07. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
 3. Bloom, Nate (2004-07-09). "Celebrity Jews". the Jewish News Weekly of Northern California. Iliwekwa mnamo 2006-07-16.
 4. Pearce, Garth. "Alyson Hannigan Interview", The Sunday Times, 2003-07-13. Retrieved on 2007-07-12. 
 5. Biography for Alyson Hannigan at the Internet Movie Database
 6. "Interview: Alyson Hannigan on American Pie". Scotland on Sunday. Aprili 22, 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-06-16. Iliwekwa mnamo 2012-06-12.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 7. "Former Atlantan Alyson Hannigan interview for 'How I Met Your Mother'". The Atlanta Journal-Constitution. Septemba 21, 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-02-22. Iliwekwa mnamo 2012-06-12.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 8. "It's Evening in America". Vanity Fair. May 2012. Page 158.
 9. "Where Are They Now? Buffy the Vampire Slayer". People. Desemba 3, 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-02-02. Iliwekwa mnamo 2012-06-12.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 10. "Alyson Hannigan, Cobie Smulders and 'Mother'-hood". USA Today. Aprili 15, 2012. Iliwekwa mnamo 2012-06-12.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 11. Wihlborg, Ulrica (2009-03-31). "Alyson Hannigan Welcomes a Daughter!". People. Iliwekwa mnamo 2009-03-31.
 12. "Alyson Hannigan and Alexis Denisof Welcome Daughter Keeva Jane". People. Juni 12, 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-01-02. Iliwekwa mnamo 2012-06-12.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 13. Hannigan is godmother of Joss Whedon's son, Alyson Hannigan.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]