Alien vs. Predator

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alien vs. Predator
Imeongozwa na Paul W.S. Anderson
Imetayarishwa na Gordon Carroll
John Davis
David Giler
Walter Hill
Imetungwa na Muswa-andishi:
Paul W.S. Anderson
Shane Salerno (uncredited)
Hadithi:
Paul W. S. Anderson
Dan O'Bannon
Ronald Shusett
Nyota Sanaa Lathan
Lance Henriksen
Raoul Bova
Ewen Bremner
Colin Salmon
Muziki na Harald Kloser
Imehaririwa na Alex Berner
Imesambazwa na 20th Century Fox
Imetolewa tar. 13 Agosti 2004
Ina muda wa dk. 101
Nchi Marekani
Bajeti ya filamu $60 million[1]
Mapato yote ya filamu $172,544,654[1]
Ilitanguliwa na Alien Resurrection
Predator 2
Ikafuatiwa na Aliens vs. Predator: Requiem

Alien vs. Predator (pia inajulikana kama AVP) ni filamu ya bunilizi ya kisayansi ya mwaka wa 2004 - kutoka nchini Marekani. Filamu iliongozwa na Paul W.S. Anderson kwa ajili ya 20th Century Fox. Igizo la filamu linatokana na nyusika mbili zilizolewa pamoja kwa ajili ya ushabiki tu wa wapenzi wa viumbe. Viumbe hivyo ni pamoja na kukutanishwa baina ya Alien na Predator, wazo ambazo linatokana na kitabu cha katuni cha mwaka wa 1989 cha "Aliens versus Predator". Anderson, Dan O'Bannon, na Ronald Shusett wametunga hadithi, na Anderson na Shane Salerno wameinakili hadithi na kuileta kwenye mtindo wa filamu. Utunzi wao uliathiriwa na hadithi za kale za Waaztec, mfululizo wa kitabu cha katuni, na tungo za Erich von Däniken.

Filamu ipo kwenye seti ya mwaka wa 2004, filamu inafuatia kikosi cha wanaakiolojia waliokusanywa na bilionea Charles Bishop Weyland (Lance Henriksen) kwa ajili ya safari ya uchungizi karibu kidogo na bara Antarctic - kuchungua dariri za joto la ajabu linalotoka huko. Weyland ana-matumaini ya kuchunguza kwa ajili yake mwenyewe, na kundi lake likagundua kwamba kuna piramid chini ya uso wa kituo cha nyangumi. Picha inayoonesha maandiko ya Wamisri ya kale na masanamu yanayonesha kwamba kule ni uwanja wa mawindo ya Mapredator ambao wanaua Maalien ikiwa kama mapambano ya kimira. Binadamu wamewekwa mtu kati wakati wa mapambano ya spishi mbili tofauti zinazojaribu kuzuia uwepo wa Maalien wasifike kwenye kilele cha uso wa dunia.

Filamu ilitolewa mnamo tar. 13 Agosti 2004, huko Amerika ya Kaskazini na imepokea tahakiki mbovu kabisa kutoka kwa watathmini wa filamu. Baadhi yao walisifia viongo maalumu na usanifu wa mahali pa kucheza filamu. Hata hivyo, Alien vs. Predator ilipata mafanikio makubwa kuingiza zaidi milioni $172 dhidi ya bajeti yake matayarisho ilikuwa $60. Mafanikio ya filamu imepelekea kutengeneza mfululizo wake wa pili mnamo 2007 iliyoitwa jina la Aliens vs. Predator: Requiem.

Hadithi[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka wa 2004, satilaiti imeona joto la ajabu linachanua chini ya Bouvetøya, kisiwa kilichopo takriban maili elfu moja kutka kaskazini mwa bara la Antarctica. Tajiri mmoja anayemiliki viwanda Charles Bishop Weyland (Lance Henriksen) amekusanya kikosi cha wanasayansi kwenda kufanya uchunguzi wa chanzo cha joto hilo na kudadi kwamba uchunguzi huo ukifanikiwa utakuwa chini ya kampuni yake ya mawasiliano ya Weyland Industries. Kikosi kimejumuisha watu wa akiolojia, wataalamu wa isimu, wana-keekee (wachimbaji mashimo), maaskari wa kulipwa, na kiongozi wa masuala ya kusafiri aliyeitwa jina la Alexa Woods (Sanaa Lathan).

Wakati ndege ya Predator inafikia katika mzingo wa Dunia, ikapasua mpini wake mmoja na kuelekea kwenye chanzo cha mchepuo wa joto. Binadamu wamefika salama kwenye eneo la juu ya chanzo cha joto, wamekuta kituo cha kusindika nyangumi kimetelekezwa, pia wamekuta mpini umezama chini ya barafu. Wakagundua kwamba pyramid ya ajabu na wakaanza kuipeleleza, wamekuta ushahidi wa ustarabu wa kuwinda uliondika historia inayoonekana kwamba mahali walipo ni pa kutolea sadaka inayotimizwa na mwana-wa-adamu na wamekuta mifupa yake.

Wakati huohuo, Predator watatu wametua katika eneo hilo na kuua wanadamu wote waliokuwa kule juu, wakaanza safari yao ya chini ya pyramid na wamewasili bila hata kikosi kujua lolote linaendelea na wakawesha umeme na mitambo ya ndani humo bila kujua. Malkia wa Alien akaamshwa kutoka kwenye mahali pa kuhifadhiwa kwenye joto dogo kabisa na kuanza kutaga mayai, mayai ambayo Alien anatotoa na wanategesha mitego kadhaa ya kunasia wanadamu ndani ya chumba cha kutolea sadaka. Alien anatokea kifuani na kukua kwa haraka zaidi na kufikia ukubwa ule unaotakikana. Utata unaanza baina ya Predators, Aliens, na wanadamu, inapelekea vifo kadhaa. Bila ya wengine kujua, Predator amepandikiza kiinitete cha Alien.

Kupitia tafsiri ya michoro ya picha za ukutani mwa pyramid wapelelezo wale wakagundua ya kwamba Mapredator hutembelea Dunia mara moja kwa miaka elfu moja. Ilikuwa kina wao waliowafunza wanadamu ustaarabu na namna ya kutengeneza mapyramid, na walikuwa wakiabudiwa kama miungu. Kila baada ya miaka 100 hutembelea Dunia - kuchukua nafasi ya mapambano ya kimira ambayo wanadamu kadhaa wanatakiwa wajitoe sadaka wenyewe wakiwa kama weneji kwa Maaliens, inatengeneza "msingi bora wa muwindwa" kwa ajili ya Predators wapate kuwinda. Iwapo watazidiwa, Mapredator watawasha silaha ya kujiangamiza mwenyewe ili Maaliens na wao wenyewe waondoshwe kabisa. Wapelelezo hao wakafikia hitimisho la kugundua kwamba ndiyo maana Mapredator wa sasa wamekuja kwenye pyramid, na hata ule mchanuo wa joto ilikuwa chambo cha kuwavutia wanadamu ili waje na waanze kusudio lao la kuwawinda Maalien.

Wanadamu waliosalia wameamua ya kwamba Maredator inabidi waruhusiwe kutimiza windo lao ili kuzuia Maalien wasifike kwenye uso wa dunia. Kadiri pambano linavyoendelea na wahusika wengi wanauawa, anabakia Alexa tu na Predator mmoja wapigane dhidi ya Maalien. Wawili wakaunda umoja na kutumia chombo cha Predator cha kujiangamiza mwenyewe ili kuangamiza pyramid na Maalien waliosalia. Alexa na yule Predator walifika juu ya uso wa dunia, ambapo walianza sheshe na Alien malkia aliotoroka. Walimshida malkia huyo kwa kuambatanisha na mnara wa tenki la maji na kumsukumia kwenye korongo lenye mimaji kwa chini, ambapo malkia yule aliburuzwa hadi chini kabisa ya bahari. Hata hivyo, yule Predator alikufa kwa majelaha yake aliyoyapata wakati wa mapambano.

Ndege ya anga ya Predator ikafichua chombo chake cha kujificha na Mapredator kadhaa wakaonekana. Wakachukua mwili wa jamaa yao aliyeuawa na kumwakilisha Alexa na moja kati ya silaha zao za mikuki ikiwa kama utambulisho kwake kama shujaa na hongera kwa maarifa yake. Kadiri wanavyorudi kwenye sayari yao, mpasua kifua anaibuka kutoka kwa Predator aliyekufa. Inanekana kwamba kutatokea chotara la Alien/Predator mwenye tabia za viumbe vyote viwili.

Washiriki[hariri | hariri chanzo]

Washiriki wengine waliocheza kwenye safu ya wapelelezi ni pamoja na Petr Jákl (Stone), Pavel Bezdek (Bass), Kieran Bew (Klaus), Carsten Voigt (Mikkel), Jan Filipensky (Boris), na Adrian Bouchet (Sven).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 "Alien vs. Predator (2004)". Box Office Mojo. Iliwekwa mnamo 21 Julai 2009.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu: