Nenda kwa yaliyomo

Lance Henriksen

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lance Henriksen

Henriksen mnamo 2010
Amezaliwa Lance James Henriksen
5 Mei 1940 (1940-05-05) (umri 84)
New York City, New York, U.S.
Kazi yake Mwigizaji, Mwigizaji Sauti Mkongwe
Miaka ya kazi 1961 – mpaka sasa
Ndoa Jane Pollack (1995-mpaka sasa)

Lance James Henriksen (amezaliwa 5 Mei 1940) ni mwigizaji wa filamu, msanii, anayefahamika zaidi na wapenzi wa TV kwa uhusika wake kwenye filamu za aina ya bunilizi ya kisayansi, aksheni na za kutisha kama vile The Terminator, na Alien, na kwenye kipindi cha TV kama vile Millennium.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Henriksen alizaliwa mjini Manhattan, New York City katika familia ya watu maskini kabisa. Baba yake alikuwa baharia wa Kinorwei na mwanamasumbwi aliyeitwa jina la utani la "Icewater" ambaye alitumia nusu ya maisha yake akiwa baharini tu. Mama'ke Henriksen alihaha kutafuta kazi akiwa kama mwelekezi wa wanengeaji, mhudumu, na mwanamitindo.[1][2] Wazazi wake walitalikiana akiwa na umri wa miaka miwili na alilelewa na mama'ke. Kadiri akuanvyo, Henriksen amejikuta akiingia katika matata mbalimbali wakatu yungali shuleni na kuthubu hata kuchungulia majumbani kwa watoto wenzi wake. Henriksen aliondoka nyumbani na kuachilia mbali shule akiwa na umri wa miaka kumi na miwili; hakujifunza kusoma mpaka alivyofikisha umri wa miaka 30, pale alipojiunza mwenyewe namna ya kusoma miswaada andishi ya filamu.[3] Ametumia ujana wake mwingi akiwa kama mtoto wa mtaani huko mjini New York. Kutembea na matreni ya mzigo nchi nzima, pia aliwekwa jela kwa makosa madogo kama vile ya uzururaji. Kilikuwa kipindi chake cha bahati kukutana na marafiki zake wa zamani Bw. James Cameron na Bruce Kenselaar.

Shughuli za uigizaji

[hariri | hariri chanzo]

Kazi ya kwanza ya Henriksen ilikuwa kwenye tamthilia na alifanya kazi kama mwandalizi wa eneo la igizo; kwa kweli, alipokea uhusika wake kwa sababu alitengeneza seti nzima ya maandalizi. Mwanzoni mwa miaka yake ya 30, Henriksen alihitimu elimu yake ya uigizaji katika chuo cha Actors Studio na kuanza kuigiza huko mjini New York City.[4] Katika filamu, ameanza kuonekana kwa mara ya kwanza kwenye filamu ya It Ain't Easy mnamo mwaka wa 1972. Henriksen akaenda kucheza katika nyusika mbalimbali na filamu pia. Nyusika hizo ni pamoja na kucheza kwenye filamu ya Steven Spielberg Close Encounters of the Third Kind (1977) na Damien: Omen II (1978). Pia amewahi kucheza kama mwanaanga Walter Schirra kwenye filamu ya The Right Stuff (1983) na mwigizaji Charles Bronson kwenye filamu ya TV mnamo 1991 - Reason for Living: The Jill Ireland Story.

Lance Henriksen akicheza kama Charles Bishop Weyland kwenye Alien vs. Predator (2004)

Wakati James Cameron anatunga filamu ya The Terminator (1984), alipanga hasa uhusika wa Terminator uchezwe na Henriksen. Cameron alikwenda mpaka akachora picha ya Terminator kwa kutumia sura ya Henriksen. Bila kujali, uhusika hatimaye ukaenda kwa Arnold Schwarzenegger. Henriksen ameonekana kwenye filamu, alicheza kwenye uhusika mdogo wa Detective Hal Vukovich. Henriksen huenda akawa anafahamika zaidi kwa kucheza kama roboti mwenye mwonekano wa binadamu, Bishop, kwenye filamu ya Aliens (1986, filamu nyingine ya Cameron) na Alien 3 (1992). Baadaye kaja kucheza kama Charles Bishop Weyland, mwonekano wa mtu uliotokana na Bishop wa awali, katika Alien vs. Predator (2004).

Filmografia

[hariri | hariri chanzo]

  • It Ain't Easy (1972) - Randy
  • To Kill the King (1974) - Hank Adams
  • Dog Day Afternoon (1975) - Murphy
  • Network (1976) - Network lawyer at Khan's place
  • Mansion of the Doomed (1976) - Dr. Dan Bryan
  • The Next Man (1976) - Federal Security
  • Close Encounters of the Third Kind (1977) - Robert
  • Damien: Omen II (1978) - Sergeant Neff
  • The Visitor (1979) - Raymond Armstead
  • The Dark End of the Street (1981) - Jimmy
  • Piranha II: The Spawning (1981) - Police Chief Steve Kimbrough
  • Prince of the City (1981) - D.A. Burano
  • A Question of Honor (1982) (TV film) - Wiley
  • Blood Feud (1983) (TV film) - Mel Pierce
  • Nightmares (1983) - MacLeod
  • The Right Stuff (1983) - Wally Schirra
  • The Terminator (1984) - Detective Hal Vukovich
  • Jagged Edge (1985) - Frank Martin
  • Streets of Justice (1985) (TV film) - Dist. Atty. Jerry Logan
  • Savage Dawn (1985) - Stryker
  • Aliens (1986) - Bishop
  • Choke Canyon (1986) - Brook Alastair
  • Near Dark (1987) - Jesse Hooker
  • Deadly Intent (1988) - Raymond
  • Pumpkinhead (1988) - Ed Harley
  • House III: The Horror Show (1989) - Detective Lucas McCarthy
  • Survival Quest (1989) - Hank
  • Johnny Handsome (1989) - Rafe Garrett
  • Hit List (1989) - Chris Caleek
  • The Last Samurai (1990) - Johnny Congo
  • The Pit and the Pendulum (1990) - Torquemada
  • Reason for Living: The Jill Ireland Story (1991) (TV film) - Charles Bronson
  • Comrades in Arms (1991) - Rob Reed
  • Stone Cold (1991) - Chains Cooper
  • Jennifer Eight (1992) - Sgt. Freddy Ross
  • Alien 3 (1992) - Bishop
  • Delta Heat (1992) - Jackson Rivers
  • Excessive Force (1993) - Devlin
  • Super Mario Bros. (1993) - The King
  • The Outfit (1993) - Dutch Schultz
  • The Criminal Mind (1993) - Agent Winslow
  • Man's Best Friend (1993) - Dr. Jarret
  • Hard Target (1993) - Emil Fouchon
  • Knights (1993) - Job
  • No Escape (1994) -The Father
  • Color of Night (1994) - Buck
  • Boulevard (1994) - McClaren
  • Spitfire (1994) - Richard Charles
  • Felony (1994) - Taft
  • Gunfighter's Moon (1995) - Frank Morgan
  • Baja (1995) - Burns
  • Aurora: Operation Intercept (1995) - William Stenghel
  • The Quick and the Dead (1995) - Ace Hanlon
  • Dead Man (1995) - Cole Wilson
  • Powder (1995) - Sheriff Doug Barnum
  • Mind Ripper (1995) (a.k.a. The Outpost) - Stockton
  • The Nature of the Beast (1995) - Jack Powell
  • Dusting Cliff 7 (1996) (a.k.a. Last Assassins) - Colonel Roger McBride
  • Profile for Murder (1997) - Adrian Cross
  • No Contest II (1997) - Eric Dane / Erich Dengler
  • The Day Lincoln Was Shot (1998) (TV film) - Abraham Lincoln

  • Tarzan (1999) - voice of Kerchak
  • Scream 3 (2000) - John Milton
  • Lost Voyage (2001) (TV film) - David Shaw
  • The Mangler 2 (2001) - Headmaster Bradeen
  • Demons on Canvas (2001) - John Soltys
  • Unspeakable (2002) - Jack Pitchford
  • The Untold (2002) (a.k.a. Sasquatch) - Harlan Knowles
  • Antibody (2003) - Dr. Richard Gaynes
  • The Last Cowboy (2003) (TV film) - John William Cooper
  • Mimic: Sentinel (2003) - Garbageman
  • The Invitation (2003) - Roland Levy
  • Rapid Exchange (2003) - Newcastle
  • Dream Warrior (2003) - Parish
  • Out for Blood (2004) (a.k.a. Vampires: Out for Blood) - Captain John Billings
  • Modigliani (2004) - Foster Kane
  • Madhouse (2004) - Dr. Franks
  • Evel Knievel (2004) (TV film) - 'Awful' Knoffel
  • Alien vs. Predator (2004) - Charles Bishop Weyland
  • Starkweather (2004) - The Mentor
  • Paranoia 1.0 (2004) (a.k.a. One Point O) - Howard
  • Into the West (2005) (TV mini-series) - Daniel Wheeler
  • Tarzan II (2005) - voice of Kerchak
  • A Message from Fallujah (2005) - Daniel Crane
  • Supernova (2005) (TV film) - Colonel Harlan Williams
  • Hellraiser: Hellworld (2005) - The Host
  • House at the End of the Drive (2006) - Skip Johansen
  • When a Stranger Calls (2006) - voice of the Stranger
  • The Garden (2006) - Ben Zachary
  • Abominable (2006) - Ziegler Dane
  • Sasquatch Mountain (2006) - Chase Jackson
  • The Da Vinci Treasure (2006) - Dr. John Coven
  • Superman: Brainiac Attacks (2006) - voice of Brainiac
  • Pirates of Treasure Island (2006) - Long John Silver
  • Pumpkinhead: Ashes to Ashes (2006) (TV film) - Ed Harley
  • Pumpkinhead: Blood Feud (2007) (TV film) - Ed Harley
  • Bone Dry (2007) - Jimmy
  • My Cousin's Keeper (2007) - Finster
  • In the Spider's Web (2007) (TV film) - Dr. Lecorpus
  • The Chosen One (2007) - Cardinal Fred (voice)
  • Deadwater (2008) (a.k.a. Black Ops) - Col. John Willets
  • Dying God (2008) - Chance
  • Dark Reel (2008) - Connor Pritchett
  • Appaloosa (2008) - Ring Shelton
  • Necessary Evil (2008) - Dr. Fibrian
  • Pistol Whipped (2008) - The Old Man (direct-to-video)
  • Prairie Fever (2008) - Monte James (direct-to-video)
  • Alone in the Dark II (2008) - Abner Lundbert (direct-to-video)
  • Ladies of the House (2008) (TV film) - Frank
  • Screamers: The Hunting (2009) - Orsow (direct-to-video)
  • The Slammin' Salmon (2009) - Dick Lobo
  • The Seamstress (2009) - Sheriff Virgil Logan
  • The Lost Tribe (2009) - Gallo
  • Jennifer's Body (2009) - Passing Motorist
  • The Genesis Code (2010) (forthcoming film) - Dr. Hoffer
  • Cyrus (2010) (forthcoming film) - Emmett
  • The Penitent Man (2010) (forthcoming film) - Mr. Darnell
  • Blood Shot (2010) (forthcoming film) - Sam
  • Wilderness (2010) (forthcoming film) - Russell Horton
  • Beautiful Wave (2010) (forthcoming film) - Jimmy
  • Godkiller (2010) (forthcoming film) - voice of Mulciber
  • Scream of the Banshee (2010)[5] (forthcoming film)

Televisheni

[hariri | hariri chanzo]
  • Ryan's Hope (1980) - Preston Post
  • Tales from the Crypt (1990) - Reno Crevice
  • Millennium (1996-1999) - Frank Black
  • The X-Files (1999) - Frank Black
  • IGPX: Immortal Grand Prix (2005) - voice of Andrei Rubley
  • Caminhos do Coração (2007) - Dr. Walker
  • Transformers: Animated (2008-2009) - voice of Lockdown
  • NCIS (2009) - Sheriff Clay Boyd
  • Verizon Droid Commercial (2010)
  1. Myatt, Sue. "Short Early Biography of Lance Henriksen", Lance Henriksen Magic, 2004-02-06. Retrieved on 2007-07-09. Archived from the original on 2007-06-17. 
  2. Lance Henriksen Biography (1940?-)
  3. Myatt, Sue. "The Web Magic Interview with Lance Henriksen: Frankly Speaking", Lance Henriksen Magic, 2004-02-06. Retrieved on 2007-07-09. Archived from the original on 2007-09-26. 
  4. Myatt, Sue. "The Web Magic Interview with Lance Henriksen: By Invitation Only", Lance Henriksen Magic, 2004-02-06. Retrieved on 2007-07-09. Archived from the original on 2007-09-26. 
  5. First Image of Lance Henriksen in 'Scream of the Banshee'!

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons