Nenda kwa yaliyomo

Piramidi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Pyramid)
Piramidi za Giza karibu na Kairo nchini Misri
(angalia jinsi watu na wanyama waonekana wadogo mbele ya majengo haya)
Piramidi za Meroe nchini Sudan

Piramidi (kutoka Kigiriki cha Kale: πυραμίδα, piramida) ni kati ya majengo makubwa kujengwa na binadamu tangu zamani. Kwa jumla piramidi ni jengo lenye msingi wa mraba na kuta zake nne zina umbo la pembetatu zikikutana juu katikati kwenye kilele.

Ingawa jamii za kale katika maeneo mbalimbali ya dunia zilijenga piramidi, zile za Misri ndizo zinazofahamika na watu wengi duniani. Piramidi zimekuwa zikitumika kama kivutio kikubwa cha utalii kwa Wamisri; hiyo imewezeshwa na uwezo wake wa kustahimili majanga tofauti na kuzisababisha ziendelee kudumu.

Piramidi za Misri zilijengwa kama makaburi ya wafalme mnamo mwaka 2000 KK. Hasa piramidi tatu kubwa za Giza karibu na Kairo zinajulikana kote duniani zikihesabiwa kuwa kati ya "maajabu ya dunia" ya kale.

Piramidi za Mesopotamia au zigurat hazikujengwa kama makaburi bali kama sehemu za makaburi ikiaminiwa ya kwamba miungu wanakaa juu yake. Mara nyingi Mnara wa Babeli unaotajwa katika Biblia (Mwanzo 11) umetazamwa ulikuwa zigurat.

Waindio wa Meksiko, hasa Wamaya na Waazteki, walijenga pia piramidi.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Piramidi kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: