Piramidi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Piramidi za Giza karibu na Kairo nchini Misri
(angalia jinsi watu na wanyama waonekana wadogo mbele ya majengo haya)
Piramidi za Meroe nchini Sudan

Piramidi (kut. Kigiriki cha Kale πυραμίδα piramida) ni kati ya majengo makubwa kujengwa na binadamu tangu zamani. Kimsingi piramidi ni jengo lenye msingi wa mraba na kuta zake nne zina umbo la pembetatu zikikutana juu katikati kwenye kelele.

Ingawa jamii za kale katika maeneo mbalimbali ya dunia zilijenga piramidi, piramidi za Misri ndizo zinazofahamika na watu wengi duniani.

Piramidi za Misri zilijengwa kama makaburi ya wafalme mnamo mwaka 2000 KK. Hasa piramidi tatu kubwa za Giza karibu na Kairo zajulikana kote duniani zikihesabiwa kuwa "maajabu ya dunia" ya kale.

Piramidi za Mesopotamia au zigurat hazikujengwa kama makaburi bali kama sehemu za makaburi ikiaminiwa ya kwamba miungu wanakaa juu yao. Mara nyingi Mnara wa Babeli unaotajwa katika Biblia (Mwanzo 11) umetazamiwa kama zigurat.

Waindio wa Meksiko hasa Wamaya na Waazteki walijenga pia piramidi.

Hourglass.svg Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Piramidi kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: