Nenda kwa yaliyomo

Ajira kwa watoto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfululizo wa sheria kuhusu ajira ya watoto, zinazojulikana kama Sheria za Kiwanda, zilipitishwa nchini Uingereza katika karne ya 19. Watoto walio na umri wa chini ya miaka 9 hawakuruhusiwa ena kufanya kazi, wale wenye umri wa miaka 9-16 wangeweza kufanya kazi saa 12 kwa siku kulingana na Sheria ya Kiwanda cha Pamba. Mnamo mwaka 1856, sheria iliruhusu ajira ya watoto wenye umri zaidi ya wa miaka 9, kwa masaa 60 kwa wiki, usiku au mchana. Mnamo mwaka 1901, umri ulioruhusiwa wa kuajiriwa kwa watoto uliongezwa hadi 12.[1][2]
Mtoto wa Kichina akitengeneza viatu, mwishoni mwa karne ya 19

Ajira kwa watoto inarejelea unyonyaji wa watoto kupitia aina yoyote ya kazi ambayo inawanyima utoto wao, inaingilia uwezo wao wa kuhudhuria shule ya kawaida, na inawadhuru kiakili, kimwili, kijamii na kimaadili.[3] Unyonyaji kama huo umepigwa marufuku na sheria duniani kote, [4] ingawa sheria hizo hazihesabu kazi zote za watoto kama ajira yao; kwa mfano kazi za usanii, majukumu ya familia, mafunzo yanayosimamiwa, na baadhi ya aina za kazi za watoto zinazofanywa kimalezi.[5] [6] Umaskini na ukosefu wa shule vinachukuliwa kuwa sababu kuu ya ajira kwa watoto. [7]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Ajira kwa watoto imekuwepo kwa viwango tofauti katika historia. Wakati wa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20, watoto wengi wenye umri wa miaka 5-14 kutoka familia maskini walifanya kazi katika mataifa ya Magharibi na makoloni yao. Watoto hao walifanya hasa kazi za kilimo, viwandani, uchimbaji madini na wengine walifanya kazi za usiku za masaa 12. Kwa kuongezeka kwa mapato ya kaya, upatikanaji wa shule na kupitishwa kwa sheria za ajira kwa watoto, viwango vya matukio ya ajira ya watoto vilipungua. [8] [9] [10]

Katika nchi maskini zaidi duniani, karibu mtoto mmoja kati ya wanne wana ajira, idadi kubwa kati yao (asilimia 29) wanaishi nchi za Afrika kusini kwa Jangwa la Sahara. [11] Mnamo mwaka 2017, mataifa manne za Afrika (Mali, Benin, Chad na Guinea Bisau) walishuhudia zaidi ya asilimia 50 ya watoto wenye umri wa miaka 5-14 wakifanya kazi. [11] Kilimo duniani kote ndicho mwajiri mkubwa zaidi wa watoto. Idadi kubwa ya ajira hizo hupatikana vijijini na katika uchumi usio rasmi wa mijini; watoto huajiriwa zaidi na wazazi wao, badala ya viwanda.

Matukio ya ajira kwa watoto yalipungua ulimwenguni kutoka 25% hadi 10% kati ya mwaka 1960 na 2003, kulingana na Benki ya Dunia. [12] Hata hivyo, jumla ya idadi ya watoto wanaotumikishwa bado ni kubwa, huku shirika la Mfuko wa Kimataifa wa Watoto (UNICEF) na Shirika la kimataifa la kazi (ILO) zikikubali wastani wa watoto milioni 168 wenye umri wa miaka 5-17 duniani kote walihusika katika ajira kwa watoto mwaka 2013. [13]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Laura Del Col (West Virginia University). "The Life of the Industrial Worker in Nineteenth-Century England". victorianweb.org.
 2. "The Factory and Workshop Act, 1901". Br Med J. 2 (2139): 1871–2. 1901. doi:10.1136/bmj.2.2139.1871. PMC 2507680. PMID 20759953.
 3. "What is child labour?". International Labour Organization. 2012.
 4. "International and national legislation - Child Labour". International Labour Organization. 2011.
 5. Larsen, P.B. Indigenous and tribal children: assessing child labour and education challenges. International Programme on the Elimination of Child Labour (IPEC), International Labour Office.
 6. "Council Directive 94/33/EC of 22 June 1994 on child labour". EUR-Lex. 2008.
 7. "Child labour - causes". ILO, United Nations. 2008.
 8. Cunningham and Viazzo (1996). Child Labour in Historical Perspective: 1800-1985 (PDF). UNICEF. ISBN 978-88-85401-27-3. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 23 Novemba 2015.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 9. Prügl, Elisabeth (1999). The Global Construction of Gender - Home based work in Political Economy of 20th Century. Columbia University Press. ku. 25–31, 50–59. ISBN 978-0231115612.
 10. Hindman, Hugh (2009). The World of Child Labour. M.E. Sharpe. ISBN 978-0-7656-1707-1.
 11. 11.0 11.1 "UNICEF Data – Child Labour". UNICEF. 2017. Iliwekwa mnamo 18 Aprili 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 12. Norberg, Johan (2007), Världens välfärd (Stockholm: Government Offices of Sweden), p. 58
 13. "To eliminate child labour, "attack it at its roots" UNICEF says". UNICEF. 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-02-25. Iliwekwa mnamo 2022-09-17.