Shirika la kimataifa la kazi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya shirila la kazi duniani

Shirika la kimataifa la kazi (kwa Kiingereza: International Labour Organization; kifupi: ILO ) ni wakala wa Umoja wa Mataifa wenye mamlaka ya kuendeleza haki za kijamii na kukuza heshima ya kazi kwa kuweka viwango vya kazi vya kimataifa (International labour standards). [1]

ILO ni shirika maalum la kwanza la Umoja wa Mataifa. Lina mataifa washirika takribani 187: 186 kati ya mataifa washirika 193 wa Umoja wa Mataifa pamoja na Cook islands. Wawakilishi wa serikali, waajiri pamoja na waajiriwa hujumuika pamoja katika kujadili na kutengeneza viwango vya kazi.

Ofisi ya kazi ya kimataifa ni sekretarieti ya kudumu ya shirika la kimataifa la kazi (ILO). Ni zingatio katika shughuli za shirika la kimataifa la kazi ambazo inaziandaa chini ya uangalizi wa bodi ya utawala ambayo inaongozwa na mkurugenzi mkuu.

Shirika la kimataifa la kazi limeajiri maafisa 2,700 kutoka mataifa yote 150 na makao makuu yake yapo Geneva, pamoja na ofisi takribani 40 kote ulimwenguni. Baadhi ya maafisa, wapatao 900, wanafanya kazi katika kitengo cha mpango wa ushirikiano wa kiufundi na miradi.

Mnamo mwaka 1969,Shirika la kimataifa la kazi lilipokea Tuzo ya Nobel ya Amani (Nobel Peace Prize) kwa kuboresha undugu na amani kati ya mataifa, na kushawishi haki ya jamii kwa wafanyakazi na kutoa msaada wa kiufundi kwa mataifa yanayoendelea. [2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Mission and impact of the ILO. ilo.org.
  2. The Nobel Peace Prize 1969. Nobelprize.org. Iliwekwa mnamo 5 July 2006.


Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu: