Bole International Airport
Mandhari
(Elekezwa kutoka Addis Ababa Bole International Airport)
Bole International Airport (kifupi cha IATA: ADD) ni uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Addis Abeba ambao ni mji mkuu wa Ethiopia.
Ni kituo kikuu cha shirika la Ethiopian Airlines na kitovu cha mtandao wa njia za ndege zake.
Uwanja huu wa ndege ulianzishwa mwaka 1961 upande wa kusini magharibi wa jiji hilo, na "Bole" ni jina la eneo lililo karibu. Wakati ule jina la uwanja wa ndege lilikuwa "Haile Selassie I International Airport" ila lilibadilishwa baada ya mapinduzi ya mwaka 1974.
Mwaka 2019 jengo jipya la kupokea abiria lilifungululiwa linalowezesha kupokea abiria milioni 22 kila mwaka.[1] Kuna barabara 2 za ndege zenye urefu wa mita 3,800.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ New terminal opens at Addis Ababa Bole International Airport, taarifa kwenye tovuti ya breakingtravelnews.com ya 31 Januari 2019, iliangaliwa machi 2019