Nenda kwa yaliyomo

Abrahamu Fukara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Abrahamu Fukara (alifariki 372) alikuwa mmonaki wa Misri katika karne ya 4 BK.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa tarehe 27 Oktoba iliyo sikukuu yake[1].

Alizaliwa Menuf (Misri) akawa kwa miaka 23 mfuasi wa Pakomi aliyeanzisha monasteri kwenye delta ya mto Nile.

Baadaye aliishi miaka 17 kama mkaapweke katika pango, lakini watu walimfahamu wakampa majina mbalimbali kama "mdogo", "mnyofu" na "fukara".

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  • Holweck, F. G., A Biographical Dictionary of the Saints. St. Louis, MO: B. Herder Book Co. 1924.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.