Yohane Maria Vianney

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtakatifu Yohane Baptista Maria Vianney.
Maiti isiyooza ya Yohane Maria Vianney.

Yohane Baptista Maria Vianney (Dardilly, 8 Mei 1786Ars-sur-Formans, 4 Agosti 1859), alikuwa padri mwanajimbo wa Kanisa Katoliki kutoka Ufaransa; kwa miaka mingi alifanya kazi ya uchungaji kama paroko wa kijiji cha Ars, huku sifa zake zikivuta watu kutoka nchi za nje ya Ulaya pia.

Alitangazwa na Papa Pius X kuwa mwenye heri tarehe 8 Januari 1905, halafu Papa Pius XI akamtangaza mtakatifu mwaka 1925 na msimamizi wa maparoko mwaka 1929.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].

Sala zake[hariri | hariri chanzo]

Nakupenda, Bwana, na neema pekee ninayokuomba, ni kwamba nikupende milele...

Mungu wangu, ikiwa ulimi wangu hauwezi kukariri kila nukta kwamba nakupenda, nataka moyo wangu ukuambie tena na tena kila ninapopumua.


Yesu wangu, jinsi inavyopendeza kukupenda!

Unijalie niwe kama wanafunzi wako juu ya mlima Tabori, nikikuona wewe tu, Mwokozi wangu.

Tuwe kama marafiki wawili ambao hata mmojawao hawezi kukubali kumchukiza mwingine. Amina.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.