Unajimu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Unajimu (wakati mwingine pia: astrolojia) ni mafundisho juu ya uhusiano kati ya nyota na maisha hapa duniani. Wafuasi wa unajimu hutangaza ya kwamba nyota zinaathiri maisha ya watu na matukio kama amani, vita au maafa.

Kuna aina nyingi za unajimu:

  • wengine wanataka kugundua mwendo wa dunia na utabiri wa mambo yajayo
  • wengine wanaamini ya kwamba tabia za mwanadamu zinatokana na hali ya nyota wakati wa kuzaliwa kwake
  • wengine wanaona nyota kama alama za miungu au nguvu za mbinguni.

Tofauti ya unajimu na astronomia[hariri | hariri chanzo]

Unajimu ni tofauti na astronomia ingawa zote mbili zilianza na kuendelea pamoja kwa karne nyingi. Tangu mwanzo wa sayansi ya kisasa wataalamu walitambua tabia za nyota kuwa magimba ya angani yenye sifa za kifizikia sio pepo, roho au miungu zinazoweza kutawala dunia au wanadamu. Kwa hiyo njia za unajimu (astrolojia) na astronomia zimeachana tangu karne kadhaa.

Asili ya unajimu[hariri | hariri chanzo]

Tangu mwanzo wa historia wanadamu katika sehemu mbalimbali za dunia walitazama nyota wakitambua nyota zinaonekana tofauti na mwendo wa majira. Walitambua pia uhusiano kati ya kuonekana kwa nyota mbalimbali na kutokea kwa mambo yaliyo muhimu kwa maisha ya kibinadamu.

Kwa mfano kuonekana kwa nyota fulani (hii inategemea mahali duniani) inaweza kuwa alama ya kwamba mvua ni karibu, au majira ya baridi inaanza. Sababu yake ni ya kwamba nyota huonekana kwa vipindi fulani wa mwaka tu; wakati wa miezi mingine zingeonekana wakati wa mchana ambako nuru ya jua inaficha nyota zote hazionekani tena. Masaa za usiku kuna vipindi ambako nyota fulani zinaonekana vizuri angani juu kabisa na kwa njia hiyo zinaweza kutambuliwa kama ishara za majira.

Watu wa kale walikuwa hodari sana kutazama nyota na kutambua mabadiliko yao katika mwendo wa wakati. Hali hii haieleweki kirahisi na watu wa leo waliozoea nuru ya taa za umeme wakitumia wakati wa usiku kutazama TV au kompyuta. Lakini kwa watu wa kale -jinsi ilivyo hadi leo kwa watu wengi vijijini au porini- nyota na mwezi zilikuwa taa hasa wakati wa usiku.

Uhusiano ulioonekana kati ya mabadiliko ya nyota na mabadiliko ya majira yalianzisha elimu ya kalenda pamoja na elimu ya unajimu na astronomia.

Kwa wazee hawa ilionekana kama nyota fulani inatawala majira, hali ya hewa na hivyo maisha ya kibinadamu kwa sababu maisha ya jamii yalitegemea majira na mwendo wa mvua, ukame, baridi au joto. Hapo ni asili ya kuziangalia nyota kama miungu au pepo zenye uwezo fulani. Hasa tabia ya hali ya hewa ya kuchelewa au kuwahi kidogo ilijenga imani ya kwamba kuchelewa kwa mvua ni dalili ya hasira ya mungu yule anayeonekana kama nyota fulani.

Horoskopi[hariri | hariri chanzo]

Kati ya mbinu za unajimu zinazojulikana sana duniani ni horoskopi. Chini ya vichwa kama "Nyota zinasema" magazeti mengi huchapisha namna za utabiri wa kila wiki kwa watu kufuatana na tarehe zao za kuzaliwa.

Icon-religion.png Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Unajimu kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.