Johannes Kepler
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Johannes Kepler (27 Desemba 1571 – 15 Novemba 1630) alikuwa mtaalamu wa falaki, hisabati na theolojia kutoka nchini Ujerumani. Amekuwa maarafu kwa sababu alitambua kanuni za mwendo wa sayari zikizunguka jua.
Alianza kazi yake kama mwalimu wa hisabati kwenye chuo cha kiprotestanti mjini Graz. Baddaye aliitwa kuja Praha alipokuwa msaidizi wa Tycho Brahe aliyekuwa mwanahisabati rasmi wa Kaisari Rudolph II na baadaye Kepler alipewa wajibu huu.
Kepler alitambua ya kwamba makadirio ya Nikolaus Koipernikus yalionyesha hali halisi maana yake sayari pamoja na dunia zinazunguka jua. Hadi wakati ule wataalamu waliamini ya kwamba dunia yetu iko katikati ya ulimwengu na jua pamoja sayari zinazunguka dunia.
[hariri] Kanuni za mwendo wa sayari
- Kanuni ya kwanza inasema sayari inatembea njia yenye umbo la duaradufu si duara kamili ikizunguka jua. Kabla ya Kepler wanafalaki waliona njia ya sayari ni duara kamili.
- Kanuni ya pili inasema ya kwamba sayari inaongeza mwendo ikikaribia jua lakini inapunguza mwendo ikienda mbali na jua.
- Kanuini ya tatu inaeleza ya kwamba sayari iliyo karibu na jua ina mkasi mkuibwa kuliko sayari mabayoo nim bali.
Kwa kanuni zake aliweza kutabiri mahali pa sayari angani vizuri kushinda wataalamu wote waliomtangulia.
[hariri] Viungo vya Nje
- Annotation: Posner Family Collection in Electronic Format Harmonices mundi ("The Harmony of the Worlds") in fulltext facsimile; Kilatini
- Electronic facsimile-editions of the rare book collection at the Vienna Institute of Astronomy
- Kepler and the "Music of the Spheres"
- Gale E. Christianson- Kepler's Somnium: Science Fiction and the Renaissance Scientist
- Kepler's Belief in Astrology by Nick Kollerstrom
- References for Johannes Kepler