Sungusila

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sungusila ni kijiji katika kata ya Nzera ya Wilaya ya Geita katika Mkoa wa Geita, Tanzania.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kijiji kilikuwa na zaidi ya wakazi wapatao 7,321 waishio humo.[1] Msimbo wa posta ni 30120.[2]

Kijiji cha Sungusila ni miongoni mwao vijiji vya Kata ya Nzera inaundwa na vijiji vya Lwenzera, Nzera yenyewe, Nyamboge, Idosera, Sungusila, na Igate.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wa kijiji hiki wengi wao ni wakulima na wafugaji.

Wakulima huzalisha mazao kama mahindi, maharage na mpunga. Mazao mengine ni pamba ambayo inafifia kwa sasa, uwele na mtama. Zao la muhogo bado ni tegemezi kwa chakula cha kila siku kwa wakazi wengi. Mazao mengine tena ni ulezi, njegere, tumbaku na karanga pia inazalisha kwa wingi matunda, hasa nanasi kijiji cha Sungusila.

Sungusila imepakana na Ziwa Victoria upande wa kaskazini mashariki na iko kandokando ya ziwa hili kubwa barani Afrika. Wakazi wengi wanajihusisha na uvuvi wa samaki kwa kutumia njia za asili zaidi. Samaki wanaovuliwa hutumika eneo lote la wilaya ya Geita na wengine husafirishwa Mwanza kwenye viwanda vya samaki. Wavuvi katika kata hii hawana elimu ya uvuvi.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Sungusila inazo shule za msingi zipatazo mbili kwa sasa.

Ikiwa imepakaba na Kijiji cha Lwenzera kinazo shule nne za Lutelangoma, Lwezear, Membe na Bweya.

Kijiji cha Nzera kina shule moja ya msingi iitwayo Nzera shule ya msingi.

Kijiji cha Nyamboge kina shule moja ya msingi iitwayo Nyamboge shule ya msingi.

Kijiji cha Idosero kina shule ya msingi Idosero.

Kijiji cha Sungusila chenyewe kina shule mbili moja iitwayo Fulwe na Sungusila.

Kijiji cha Igate kinayo shule moja iitwayo Igate shule ya msingi.

Vijiji vyote hivi vitano vinategemea shule moja tu ya sekondari iitwayo Bugando Secondary. Shule hiyo ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 700 kwa mwaka kati ya wahitimu zaidi ya 600 wanaohitimu na kufaulu kila mwaka. Ilianzishwa mwaka 1998 kama shule ya kutwa.

Afya[hariri | hariri chanzo]

Sungusila inacho kituo kimoja cha afya cha fulwe

Watu maarufu wa kijiji hicho=[hariri | hariri chanzo]

Kijiji cha Sungusila wakazi wake wengi ni Wasukuma japo kuna makabila mengine pia madogo madogo ambayo si asili ya kijiji hicho kama wazinza, Wajita, Waha

Watu maarufu katika kijiji hicho ni:

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sensa ya 2012, Geita Region – Geita District Council
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01. 
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Geita bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.