Waha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Waha ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Kigoma, pia mpakani na Burundi. Lugha yao ni Kiha

Kabila la Waha limetokana na mtawanyiko wa makabila ya Warundi na Wahaya, kipindi cha kuhamahama kwa ajili ya kutafuta masilahi kama vile chakula na vita. Baada ya kufika kandokando mwa ziwa Tanganyika na maeneo yote yanayolizunguka Ziwa Tanganyika waliweza kukaa na kuanzisha shughuli mbalimbali kama vile kilimo, uvuvi, ufugaji na uwindaji.

Waha walipoanza kuyazoea mazingira, walijigamba na kujidai kwa makundi ya kikoo kuwa yana nguvu, kila mmoja kwa nafasi yake, na kila ukoo ulijigamba kwa kutumia majina ya wanyama, wadudu, ndege milima n.k, mfano, kuna waliokuwa wakijigamba kuwa wao ni WASHUBHI ambao walijulikana kwa mnyama ambaye ni Kondoo yaani wapole, Sisimizi(Chunguchungu) Walijigamba kama Wakulima, wengine kama konoo, kiboko, n.k, na walijulikana tabia zao kulingana na majina ya ukoo wao.

Kilimo cha Waha ni Mahindi, maharage, ndizi, kahawa, mhogo, karanga, mbaazi, njegere, viazi mviino, viazi vitamu, mtama, ulezi, mahore, miwa, mpunga,korosho,n.k

Pia Waha ni wavuvi wa samaki katika ziwa Tanganyika, mto Malagarasi, Mto Rwiche, Mto Mkoza, Na Mito minin midogomidogo kama vile, Nyajijima, Mresi, Kazingu, n.k

Waha ni wafugaji wa N'gombe, mbuzi, kuku, bata, Nguruwe, sungura, mbwa paka, n.k,

Biashara zao ni Mazao wanayoyalima, samaki, na bidhaa nyingine za kawaida. Usafiri wao wa asili ilikuwa na Miguu yao wenyewe, ambapo kuna imani ilikuwepo pia ambayo ni yakusadikika kuwa walitumia UNGO kusafilia kama ndege yao ya asili.

Utamaduni wao, yaani mavazi yao ilikuwa ni magome ya miti yaliyojulikana kama mpuzu, na nyumba zao ni za msonge, udongo na miti, kulingana na sehemu mbalimbali, mana kuna sehemu zenye joto kama vile nyanda za jini au bondeni, na sehemu zenye baridi kama vile nyanda zenye joto.