Raphael
Raffaello Sanzio (anajulikana kama Raffael au Raphael) (6 Aprili 1483 - 6 Aprili 1520) alikuwa mchoraji na mjenzi kutoka Italia.
Pamoja na Leonardo da Vinci na Michelangelo huhesabiwa kati ya wasanii muhimu wa zama ya mwamko ya Italia.
Alizaliwa mjini Urbino kwa hiyo huitwa pia Raffaello da Urbino au Raffaello Sanzio da Urbino.
Maisha[hariri]
Raphael alizaliwa kama mtoto wa mchoraji Giovanni Santi aliyefanya kazi katika utumishi wa mkabaila Federiko III wa Montefeltro.
Katika umri wa miaka 15 alikuwa mwanafunzi katika karakana ya mchoraji Pietro Perugino aliyeshiriki katika kazi za kupamba Kikanisa cha Sistina kwenye Vatikano.
Raphael alijifunza haraka na tangu 1500, alipokuwa na umri wa miaka 17, alipewa kazi za kwanza za kujitegemea.
Alianza kuchora picha katika makanisa ya miji mbalimbali ya Italia.
Alipenda kutembelea Firenze akitazama michoro ya walimu wa kale.
Tangu alipohamia Roma alikoitwa na Papa Julius II, kazi kubwa aliyopewa ilikuwa picha za ukutani kwenye vyumba vya Papa mwenyewe.
Raphael aliaga dunia mapema katika umri wa miaka 37. Hakuoa wala hakuna watoto waliojulikana.
Picha za Raphael[hariri]
-
Picha ya Baldassare Castiglione, (1514-1515)
-
Picha ya Guidobaldo wa Montefeltro, Palazzo degli Uffizi huko Firenze
-
Picha ya Papa Julius II, (1511-1512)
-
Mt. Sebastiano
-
Maria na mtoto Yesu
-
Maria na mtoto Yesu (mnamo 1507)
-
Picha ya Agnolo Doni, (1506), Firenze
-
Picha ya Maddalena Doni, (1506)
-
Picha ya mwanamke aliyeitwa "La Muta", Galleria Nazionale delle Marche mjini Urbino
-
Mt. George akipigana na joka (1505)
-
Picha ya Francesco Maria della Rovere] (1514), (Czartoryski Museum), Kraków (Polandi)
Viungo vya Nje[hariri]
- (Kifaransa) Picha kadhaa za Rapahel
- (Kifaransa) Tovuti ya kibiashara inayoonyesha picha 275 za Raffaello Santi
- (Kiingereza) Raphael kwenye Artcyclopedia