Peter I wa Urusi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tsar Peter I wa Urusi
Tsar Peter I wa Urusi

Peter Mkuu ni jinsi Tsar (au Kaisari) Peter I wa Urusi anaitwa mara nyingi. Jina lake la Kirusi lilikuwa Pyotr Alekseyevitch Romanov (Пётр Алексеевич Романов). Aliishi 1672 hadi 1725. Alikuwa mtawala aliyefikisha Urusi yenye historia ya Kiasia katika siasa na utamaduni wa Ulaya.

Peter Mkuu alianza utawala wake mwaka 1689 akiwa na umri wa miaka 17. Mwanzoni alilenga kuimarisha jeshi la Urusi na hasa wanamaji. Akiona ya kwamba mafundi wote wa kujenga meli walitoka Ulaya hasa Uholanzi alifanya safari akakaa Uholanzi na kuwa mfanyakazi wa kujenga jahazi kwa miezi minne.

Aliporudi kutoka safari hii alikuwa na wazo ya kwamba nchi yake Urusi ulikuwa nyuma sana kulinganisha na nchi za Ulaya alianza mipango mini ya kuleta maendeleo Urusi. Aliamuru waungawana wote kwake kwenye jumba la kifalme kukata ndevu zao na kuvaa nguo za Kiulaya. Alialika mafundi na wataalamu wengi kutoka Ulaya.

Hasa alianza kujenga mji mkuu mpya kwenye mwambao wa Baltiki yaani katika pemba la magharibi kabisa ya milki yake. Mji huu uliitwa Sankt Peterburg ukachukua nafasi ya Moskva kunanzia 1712 hadi 1918.

Katika vita mbalimbali alivunja nguvu ya Uswidi na kutwaa majimbo mapya ya Estonia na Latvia.

Alibadilisha pia mfumo wa utawala wa kanisa la Kiorthodox la Urusi. Aliondoa cheo cha Patriarka (Askofu Mkuu) na badala yake aliunda ofisi ya Sinodi Kuu iliyokuwa mkono wa serikali yake.

Image:WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Peter I wa Urusi" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Peter I wa Urusi kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.

Vifaa binafsi
Lugha nyingine