Nenda kwa yaliyomo

Mercy Nenelwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru




Mercy Nenelwa
Nchi Tanzania
Kazi yake Mfanyabiashara na mjasiliamali

Mercy Nenelwa ni mfanyabiashara na mjasiriamali kutoka nchini Tanzania.

Kwa sasa ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Nelwa inayojishughulisha na utengenezaji wa Ice cream. Jina lake la kazi anaitwa Nelwa's Gelato ambalo limetokana na jina la baba yake na Gelato inamaanisha icecream kwa lugha ya Kiitalia.[1]. Nelwa hutumia uzalishaji wa barafu nchini Tanzania kujifunza faida anayoipa ili kuongeza elimu yake ya uzalishaji na ujasiriamali nchini.[2]

Maisha yake

[hariri | hariri chanzo]

Mercy Nenelwa alizaliwa nchini Lesotho na kusoma shule ya kimaitaifa ya Arusha na baadaye sekondari ya Kiraeni iliyopo Wilaya ya Rombo, mkoa wa Kilimanjaro na kumaliza kidato cha sita shule ya sekondari ya Morogoro. Mercy ana shahada ya kwanza ya Masuala ya Biashara

Mercy Nenelwa Kitomari ana uzoefu wa zaidi ya miaka mitano ya uzalishaji wa kiwanda cha ice cream. Mwanzoni alikuwa mwanzilishi na CEO of Notre Héritage LTD, ambayo inajihusisha na uzalishaji na usambazaji wa ice cream za nyumbani ambazo zinajulikana kama Nelwa's Gelato.

Mercy pia ana vifaa vya kutengeneza vikapu vya barafu kama sehemu ya mipango yake ya ujasiriamali wa vijana katika Kanisa la DPC na hutumika kama mshauri wa Mkutano wa Vijana.

Kama mjasiriamali wa kike, Mercy ana motisha ya kushawishi Wanawake wenzake kuwa na maarifa na ujuzi wake na kuhamasisha wanawake wengine kufuata ndoto zao. Pia ana nia ya kurekebisha sekta ya barafu katika bara la Afrika kupitia darasa lake la ice cream101.

Baada ya kukamilika kwa Fellowship ya Mandela Washington, Mercy ana mpango wa kuendeleza kazi yake ya kuwashauri wajasiriamali zaidi katika sekta ya barafu, na kuendeleza mpango wa vijana wa kudumu na vijana wa DPC wanaopenda biashara.

Historia ya biashara yake

[hariri | hariri chanzo]

Wazo la ice cream lilikuja kipindi Mercy akisoma huko London na kufanya kazi yake ya muda ilikuwa kupeleka watoto kula ice cream na anasema kulikuwa na foleni ikawa ni shida; basi akawaza kuwa huku kuna baridi hivi na ice cream zinaliwa sana kumbe Dar es Salaam ni joto mwaka mzima: naweza kuuza sana Dar kwa kuwa wazalishaji wa icecream ni wachache. Alichukua muda wa kwenda kusomea kabisa mwaka 2011 kutengeneza ice cream na alifanya kazi ya kujitolea ili tu ajifunze. Akaanza rasmi mwaka 2012 kwa kutengenezea marafiki zake na familia yake huku akiwa anafanya kazi Exim Bank. Mnamo Septemba 2013 akaacha kazi huko benki akaaamua kutengeneza ice cream.[3]

Tuzo alizopata

[hariri | hariri chanzo]

Mercy Nenelwa ameweza kupewa tuzo kadhaa ambazo zinatambua kazi yake na mchango wake, ikiwa ni pamoja na mjasiriamali wa mwaka, mwanzo wa mwaka, na bidhaa zenye ubora wa hali ya juu Tanzania. Pia amekuwa anajihusisha katika masuala mengi ya vyombo vya habari, kama CNN na BBC ambavyo viliweza kumuonyesha ufanisi wake wa ujasiriamali. [4]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-23. Iliwekwa mnamo 2018-09-08.
  2. https://aim2flourish.com/innovations/gelato-natures-guilty-pleasure
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-23. Iliwekwa mnamo 2018-09-08.
  4. https://cwrutanzania2018.weebly.com/dar-es-salaam/nelwas-gelato
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mercy Nenelwa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.