Leonardo wa Portomaurizio
Leonardo wa Portomaurizio (Porto Maurizio, leo Imperia, 20 Desemba 1676 - Roma 26 Novemba 1751), alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo na padri wa Kanisa Katoliki.
Ni maarufu hasa kwa mahubiri yake ya wiki nzima aliyoyaendesha karibu mfululizo nchini Italia, akisisitiza hasa ibada kwa mateso ya Yesu kwa kupitia vituo 14 vya njia ya msalaba.
Papa Pius VI alimtangaza mwenye heri, halafu Papa Pius IX akamtangaza mtakatifu tarehe 29 Juni 1867.
Sala yake[hariri]
Yesu wangu, kwa haki tu na kwa shukrani napaswa kujitoa kabisa kwako, baada ya wewe kujitoa kabisa kwangu...
Wewe umetakasa hisi zangu zote; fanya ziwe zako, zisifurahie tena kilicho kinyume cha sheria yako ya Kimungu.
Umetakasa kumbukumbu yangu; iwe inakukumbuka mfululizo.
Umetakasa utashi wangu; usigeuke kamwe kupenda chochote kuliko wewe.
Basi, kutoka dhati ya moyo wangu nakutolea kama sadaka kamili ya kudumu, kadiri ninavyoweza, mwili wangu na roho yangu, hisi zangu na vipawa vyangu, nilichonacho na jinsi nilivyo.
Ee moto wa Kimungu, choma, Ee Upendo wa Mwenyezi, choma na kuteketeza yale yote yasiyo yako ndani mwangu! Amina.
Marejeo[hariri]
- Summarium processus beatificationis V.S.D. Leon. a P.M. (Rome, 1781)
- RAFELLO DA ROMA, Vita del P. Leonardo da P.M. (Rome, 1754)
- JOS. De MASSERANO, Vita del B. Leonardo da P.M. (Rome, 1796), written by the postulator and dedicated to the duke of York, son of James [III] of England
- SALVATORE DI ORMEA, Vita del B. Leonardo da P.M. (Innsbruck, 1869)
- L. De CHERANCE, S. Leonard de Port-Maurice (Paris, 1903) in Nouvelle Bibliothèque Franciscaine (1st series), XIII. Chapter xx of this last mentioned work had already appeared in Etudes Franciscaines, VIII (Paris, 1902), 501-10.
Viungo vya nje[hariri]
- Life of St. Leonard of Port-Maurice, O.F.M.
- Catholic Encyclopedia: St. Leonard of Port Maurice
- St. Leonard of Port Maurice - AmericanCatholic.org
| Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Leonardo wa Portomaurizio kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |