Ignas wa Antiokia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kifodini cha Mt. Ignas.

Ignas wa Antiokia (kwa Kigiriki Ἰγνάτιος, Ignatios: lakini alijulikana pia kwa jina la Θεοφόρος, Theophoros, yaani "Mleta Mungu") alizaliwa kati ya miaka 35 na 50 B.K. akafa kati ya 98 na 117.[1]

Ni kati ya Mababu wa Kanisa wa kwanza, akiwa mwanafunzi wa Mitume wa Yesu na askofu wa tatu wa Antiokia, leo nchini Uturuki.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake inaadhimishwa na Wakatoliki[2][3], Waanglikana na Waorthodoksi wa Mashariki kwenye 17 Oktoba, lakini na Waorthodoksi tarehe 20 Desemba.

Maandishi yake[hariri | hariri chanzo]

Akielekea kifodini chake huko Roma, aliandika barua kadhaa kwa makanisa na kwa Polikarp Mtakatifu ambazo 7 za hakika zimetunzwa kama kielelezo cha teolojia ya awali ya Ukristo. Humo kwa mara ya kwanza tunasoma juu ya Kanisa Katoliki ambalo linaitwa hivi kwa kulitofautisha na makundi ya Wakristo waliotengana nalo.

Kati ya mada muhimu zaidi kuna Kanisa, sakramenti na nafasi ya askofu pekee katika kila jimbo.

Barua zake zimetafsiriwa kwa Kiswahili na kutolewa Italia kama ifuatavyo: MT. IGNASI WA ANTIOKIA, Nyaraka - tafsiri ya B. Santopadre n.k. – ed. E.M.I. – Bologna 1992 – ISBN 88-307-0404-0

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Tazama: "Ignatius" katika The Westminster Dictionary of Church History, ed. Jerald Brauer (Philadelphia:Westminster, 1971) na pia David Hugh Farmer, "Ignatius of Antioch" katika The Oxford Dictionary of the Saints (New York: Oxford University Press, 1987).
  2. Calendarium Romanum (Vatican City, 1969)
  3. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.