Chama cha Kikristo cha Kidemokrasia cha Ujerumani
| Christlich Demokratische Union Deutschlands | |
|---|---|
| Kiongozi | Dk. Angela Merkel (Chansela) |
| Kimeanzishwa | 1870 (Kama Centre Party) 1945 (CDU) |
| Makao Makuu | Klingelhöferstraße 8 10785 Berlin |
| Itakadi ya Chama | Christian Democracy, Conservatism |
| Ushirikiano wa Kimataifa | Christian Democrat International na International Democrat Union |
| Ushirikiano kwa Ulaya | {{{Ulaya}}} |
| Kundi la Ubunge wa Ulaya | {{{bunge la ulaya}}} |
| Rangi | Black, Orange |
| Tovuti | www.cdu.de |
| Tazama pia | Siasa ya Ujerumani |
Chama cha Kikristo cha Kidemokrasia cha Ujerumani au Christlich Demokratische Union Deutschlands (CDU) ni moja kati ya vyama viwili vikubwa vya kisiasa nchini Ujerumani. Kinajielezea chenyewe kuwa:
chama cha kisiasa kilicho cha Kikristo, cha kidemokrasia, cha uhuru na cha mapokeo, chenye msimamo wa kati ya eneo la kisiasa.
Mnamo mwezi Novemba katika mwaka wa 2005 Bi. Angela Merkel amepata kuwa Chansela wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kwa kupitia kiti cha chama cha CDU.
Chama na dini [hariri]
Kihistoria CDU ilianzishwa kama maungano ya mikondo ya kikatoliki na kiprotestanti ya sisasa ya Kijerumani baada ya vita kuu ya pili ya dunia. Kabla ya utawala wa Adolf Hitler mikondo hii iliendelea kandokando hadi 1933; chama cha Zentrum ilikuwa chama cha kikatoliki na vyama vya kiprotestanti vilijipasua hadi kupotea. Baada ya vita ilikua nia ya wanasiasa Wakristo kuungana kwa sauti moja hivyo waliunda CDU. Kwa miaka mingi uwiano kati ya wanasiasa wakatoliki na waprotestanti ilikuwa jambo muhimu ndani ya chama.
Katika miaka ya nyuma CDU imejitahidi kukusanya pia Waislamu Wajerumani hasa kutoka wahamiaji Waturuki na watoto wao. CDU imekuwa chama cha kwanza katika Ujerumani kilichomteua waziri mwislamu kwenye ngazi ya serikali ya jimbo la Saksonia ya chini mwaka 2010.
| Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |