Nenda kwa yaliyomo

Kindi Mrukaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Zenkerella)
Kindi mrukaji
Kindi mrukaji wa Pel (Anomalurus pelii)
Kindi mrukaji wa Pel (Anomalurus pelii)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wagugunaji)
Nusuoda: Anomaluromorpha (Wanyama kama kindi warukaji)
Familia: Anomaluridae
Gervais, 1849
Ngazi za chini

Jenasi 3, spishi 7:

Kindi warukaji ni wanyama wadogo hadi wakubwa kiasi wa familia Anomaluridae. Wanatokea misitu ya Afrika kusini kwa Sahara. Kuna kindi warukaji huko Asia pia, lakini jamii hizi hazina mnasaba. Wale wa Afrika wana ngozi kati ya miguu ya mbele na ya nyuma, isipokuwa spishi moja, kindi mkia-magamba. Upande wa chini wa msingo wa mkia wao mrefu una mistari miwili ya magamba yenye ncha kali yanayomsaidia mnyama ili kupanda juu ya miti. Rangi yao ni kijivu, kahawia, kahawiachekundu au hudhurungi. Hula matunda, makokwa, maua na majani na pengine wadudu pia.

Spishi ya kabla ya historia

[hariri | hariri chanzo]
  • Kabirmys qarunensis (Mwisho wa Eocene ya Birket Qarun, Misri)