Zap Mama

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Zap Mama wakiwa wanatumbuiza katika klabu ya mjini Baltimore, Maryland kunako tar. 1 Novemba ya mwaka wa 2007. Kutoka kushoto ni: Marie Daulne, kiongozi na ndiyo mwanzilishi wa kundi la Zap Mama, anayeonekana kwa kati.

Zap Mama ni kikundi cha muziki cha Kibelgiji kilicho anzishwa na kuongozwa na mwanamama Marie Daulne. Daulne alisema kwamba yeye mpango wake ni kuwa kama daraja baina ya watu wa Ulaya na Waafrika na kuzileta tamaduni zote mbili pamoja kwa kutumia muziki wake.[1] "Kitu ambacho nilichokuwa napenda kukifanya ni kuleta midundo ya Kiafrika na kuipeleka katika dunia ya Kimagharibi, kwasababu naamini kupitia muziki na midundo yake, watu watagundua tamaduni mpya, watu wapya na dunia mpya."

Zap Mama hupiga muziki mchanganyiko ikiwemo muziki wa Kiafrika, R&B, na Hip-hop na kuzilekezea sauti katika namna ya muziki wao wanavyoupiga.

"Sauti huwa zinafanya midundo zenyewe," alisema Daulne. "Ni midundo asilia. Misingi ya midundo. Midundo ya kupendezesha nafsi, sauti ya wanadamu. "Zap Mama huwa wanaimba kwa lugha ya Kifaransa, Kiingereza na Kiafrika zaidi.

Albamu za muziki[hariri | hariri chanzo]

Discography[hariri | hariri chanzo]

  • Zap Mama (1991)
  • Adventures in Afropea (1993)
  • Sabsylma (1994)
  • Seven (1997)
  • A Ma Zone (1999)
  • Ancestry in Progress (2004)
  • Supermoon (2007)

Zap Mama pia walishiriki katika kutengeneza kibwagizo cha filamu ya Mission Impossible 2 na Iko-Iko (1999).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]