Youlou Mabiala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Gilbert Youlou Mabiala (alizaliwa 3 Machi, 1947), maarufu kama Prince Youlou, ni msanii wa muziki wa Kongo, mtunzi na mwimbaji, katika Jamhuri ya Kongo (Congo-Brazzaville). Aliwahi kuwa mwanachama wa bendi ya muziki wa Kongo ya TPOK Jazz ambayo ilikua maarufu katika muziki wa Kongo kuanzia miaka ya 1960 hadi 1980.

Kazi ya muziki na OKJazz[hariri | hariri chanzo]

Youlou Mabiala alizaliwa Linzolo, kitongoji cha Brazzaville, mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo. Alianza kazi yake ya muziki huko Brazzaville na vikundi vya ndani. Mnamo 1963, alijiunga na bendi ya muziki ya TPOK Jazz, huko Kinshasa (Leopoldville), kama mwimbaji na mtunzi. Baada ya misukosuko ya hatua ya awali, aliishi chini ya malezi ya Vicky Longomba .

Youlou Mabiala anasifika kwa kutunga nyimbo zifuatazo za bendi:

  • Celine
  • Kamikaze
  • Asumani [1]
  • Ledi
  • Massi
  • Lekwey (Franco na Youlou)

Mnamo 1972, Youlou alikuwa mmoja wa wanamuziki waliohama kutoka bendi ya OKJazz na kuanzisha bendi iliyojulikana kama Lovy du Zaïre, iliyoongozwa na Vicky Longomba.

Alirejea tena katika bendi ya OKJazz mwaka 1975 na kuachia kibao cha Kamikaze ambacho kilikuwa maarufu barani Afrika na miongoni mwa wanadiaspora wa Afrika barani Ulaya na Amerika Kaskazini. Mnamo 1977, Youlou aliondoka OKJazz kabisa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Siddikh, Aboubacar (30 June 2008). "Asumani (Youlou Mabiala) - T.P. O.K. Jazz Télé Zaire 1975". Youtube.com. Iliwekwa mnamo 13 April 2014.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Youlou Mabiala kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.