Yombo Vituka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Kata ya Yombo Vituka
Kata ya Yombo Vituka is located in Tanzania
Kata ya Yombo Vituka
Kata ya Yombo Vituka

Mahali pa Yombo Vituka katika Tanzania

Majiranukta: 6°52′8″S 39°15′40″E / 6.86889°S 39.26111°E / -6.86889; 39.26111
Nchi Tanzania
Mkoa Dar es Salaam
Wilaya Temeke
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 59,975

Yombo Vituka ni jina la kata ya Wilaya ya Temeke katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania yenye postikodi namba 15115[1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ina wakazi wapatao 59,975 waishio humo.[2] Yombo Vituka awali kwenye miaka ya 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990 ilikuwa na eneo kubwa la mashamba ya watu ya miembe, mikorosho, mpunga, na kadhalika. Lakini kuanzia miaka ya 1995 na kuendelea, kata imeanza kupanuka kwa kiasi kikubwa sana na kupelekea kuwa na majumba mengi ya watu wenye uwezo. Leo hii, Yombo Vituka imekuwa sehemu yenye wakazi wengi kupita hata kata zake za jirani kama vile Kiwalani na Kitunda.

Eneo la Yombo Relini. Kwa mbali unaona soko dogo ambalo linahudumia wakazi wa Vituka na Kiwalani kwa ujumla wake.

Marejeo

Kata za Wilaya ya Temeke - Tanzania

Azimio | Buza | Chamazi | Chango'mbe | Charambe | Keko | Kibondemaji | Kiburugwa | Kijichi | Kilakala | Kilungule | Kurasini | Makangarawe | Mbagala | Mbagala Kuu | Mianzini | Miburani | Mtoni | Sandali | Tandika | Temeke | Toangoma | Yombo Vituka