Wilfried Zaha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wilfried Zaha

Dazet Wilfried Armel Zaha alizaliwa tarehe 10 Novemba mwaka 1992.Ni mchezaji wa soka anayecheza kama mshambuliaji katika klabu ya Crystal Palace na timu ya taifa ya Ivory Coast.

Zaha alijiunga na timu ya Crystal Palace kutoka katika kituo cha kufundishia soka mwaka 2010. Katika msimu wake wa kwanza alifunga mabao 18 katika mashindano yote. Mnamo Januari 2013, alihamishiwa Manchester United kwa ada ya awali ya £ 10 milioni (mchezaji wa gharama kubwa zaidi wa Crystal Palace aliyeuzwa wakati huo). Zaha alirudi Palace Agosti 2014 kwa mkopo wa muda mrefu, kabla ya kusaini mkataba wa kudumu mwezi Februari 2015. Tangu wakati huo alikuwa mchezaji wa 12 mwenye mabao mengi kwenye klabu hiyo.[1]

Alizaliwa nchini Ivory Coast, na alikulia Uingereza akiwa na umri wa miaka minne. Alichezea timu ya taifa ya Uingereza mwaka 2012, akionekana katika mechi mbili zisizo za ushindani. Baada ya kutochezea Uingereza kwa miaka minne, alijiunga na timu ya taifa ya Ivory Coast kabla ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2017.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. www.holmesdale.net, Holmesdale Online. "All-time top scorers". Holmesdale Online. Iliwekwa mnamo 2020-12-09.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wilfried Zaha kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.