Wileadi wa Bremen
Mandhari
(Elekezwa kutoka Wileadi wa Brema)
Wileadi wa Bremen (pia: Vilhaed, Willehad, Willihad; Northumberland, 740 hivi - Blexen, 8 Novemba 789) alikuwa padri wa Uingereza rafiki wa Alkwino wa York.
Mwaka 766 alitumwa kama mmisionari huko Frisia na Saksonia, katika Uholanzi na Ujerumani wa leo, kuendeleza kazi ya Bonifas mfiadini[1].
Baada ya kupata mateso mbalimbali, hatimaye akawa askofu wa kwanza wa jimbo la Bremen akaliongoza kwa busara [2].
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na wengineo kama mtakatifu.
Sikukuu yake ni tarehe 8 Novemba ya kila mwaka[3].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- McKitterick, Rosamond (1983). The Frankish Kingdoms under the Carolingians, 751–987. London: Longman.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Saint of the Day, November 8: Willehad of Bremen Ilihifadhiwa 30 Desemba 2019 kwenye Wayback Machine. at SaintPatrickDC.org
- Willehad Ilihifadhiwa 10 Januari 2007 kwenye Wayback Machine. at Patron Saints Index
- Bishopric of Bremen
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |