Wafrisia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maeneo yaliyokaliwa na Wafrisia kihistoria
"Nederlande" = Uholanzi; "Deutschland" = Ujerumani

Wafrisia ni kundi la watu wanaoishi katika Uholanzi ya mashariki na Ujerumani ya Kaskazini karibu na pwani ya Bahari ya Kaskazini katika maeneo ya Frisia ya kihistoria, yakiwa pamoja na mkoa wa Friesland wa Uholanzi, wilaya ya Friesland katika Saksonia Chini, Ujerumani, na wilaya ya Nordfriesland (Frisia Kaskazini) katika Schleswig-Holstein, Ujerumani.

Lugha ya kienyeji ni Kifrisia ambayo ni lugha ya Kigermanik iliyo karibu na Kiingereza. Idadi ya wasemaji imepungua, na leo hii wakazi wengi wa maeneo ya Frisia wanatumia ama Kiholanzi na Kijerumani au lahaja mojawapo ya Kijerumani cha kaskazini.

Katika historia Wafrisia walijulikana tangu siku za Dola la Roma yaani takriban miaka 2000 iliyopita.