Kahama (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wilaya ya Kahama Mjini)


Kata ya Kahama
Nchi Tanzania
Mkoa Shinyanga
Wilaya Kahama
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 32,345

Kahama ni manisipaa[1] iliyo kaskazini magharibi mwa Tanzania na yalipo makao makuu ya wilaya ya Kahama Mjini katika Mkoa wa Shinyanga, wenye halmashauri yake ya pekee hivyo yenye hadhi ya wilaya. Halmashauri ilianzishwa baada ya kugawa kwa Wilaya ya Kahama ya awali. Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa watu 242,208. [2]

Mji huu ni maarufu kwa uchimbaji wa dhahabu. Pia ni mji wa pili kwa mapato kati ya halmashauri za wilaya, ikitanguliwa na Kinondoni na kufuatiwa na Mufindi.

Tangu 1984 mji umekuwa makao makuu ya dayosisi ya Kahama ya Kanisa Katoliki.

Ramani ya eneo la Kahama Tanzania

Mahali ilipo[hariri | hariri chanzo]

Kahama ipo takriban kilomita 109 sawa na maili 68 umbali kwa barabara kutokea kusini magharibi mwa Shinyanga ambapo makao makuu ya mkoa yanapatikana.[3] pia ni takriban kilomita 536 sawa na maili 333 umbali kwa barabara kutokea kaskazini magharibi mwa Dodoma ambao ndio mji mkuu wa Tanzania.[4]

Idadi ya watu[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2006 ilikadiriwa kuwa na idadi ya watu 36,000.[5]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Kahama Mjini - Mkoa wa Shinyanga - Tanzania

Busoka | Isagehe | Iyenze | Kagongwa | Kahama Mjini | Kilago | Kinaga | Majengo | Malunga | Mhongolo | Mhungula | Mondo | Mwendakulima | Ngogwa | Nyahanga | Nyandekwa | Nyasubi | Nyihogo | Wendele | Zongomera

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Shinyanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kahama (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.