Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Ukufunzi (Viungo vya Wikipedia)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Utangulizi   Kuhariri   Kuanzisha Makala   Muundo   Viungo vya Wikipedia   Kutaja vyanzo   Kurasa za majadiliano   Kumbuka   Kujisajili    

Kuunga pamoja viungo vya makala za Wikipedia ni kazi nyepesi lakini muhimu sana. Inaruhusu watumiaji kupata habari nyingi zinazohusiana na makala wanayosoma. Inaongeza manufaa ya Wikipedia kwa wasomaji.

Mfano

Viungo vya buluu

Makala juu ya mji wa Misri inaweza kuonekana hivyo:

Giza (Kar.: الجيزة al-gīza) ni mji wa kaskazini ya Misri unaopakana na mji mkuu Kairo. Inajulikana hasa kama mahali pa piramidi.

Maneno yenye rangi ya buluu yamepewa kiungo kwenda makala mengine kuhusu Kar. = Kiarabu, Misri, Kairo na piramidi.

Viungo vyekundu

Kuna pia viungo vyenye rangi nyekundu:

Mabata-bahari ni ndege wa maji wa familia ndogo ya Merginae katika familia ya Anatidae.

Katika sentensi hii makala za ndege, Merginae na Anatidae ziko tayari lakini "familia ndogo" na "familia (biolojia)" hazikuandikwa bado. Wakati wa kuandika makala unaweza kuanzisha viungo vyekundu ukiona hapa ni neno muhimu inayostahili makala yake.

Hapa unatakiwa kuwa kiangilifu

  • usiweke maneno hovyo katika mabano mraba na kuanzisha kiungo chekundu
  • fanya utafiti kama mada iko tayari labda kwa tahajia tofauti; kwa mfano umetafuta nchi ya "Aljiria" lakini kumbe: "Algeria" iko tayari!

Jinsi ya kuunga

Mabano mraba [[]]

Kuweka kiungo kwenda ukurasa mwingine wa Wikipedia (inaitwa kiungo cha wiki), weka katika mabano mraba mawili, kama hivi:

Mfano: [[Televisheni]] = Televisheni.

Kigawanyishi-kibomba "|" kwa umbo tofauti la neno

Mara kwa mara jina la makala inayoelekezwa ni tofauti kidogo na maneno katika makala unayoshughulikia kama tofauti umoja/uwingi.

Mfano: "Serengeti kuna viboko wengi...". Unataka kuweka kiungo kwenda makala ya mnyama "kiboko".

Hapa unaweza kugawa mabano mraba kwa kutumia alama ya kigawanyishi-kibomba "|" (SHIFT + BACKSLASH kwenye baobonye zenye ABC za Kiingereza). Sasa kuna sehemu mbili ndani ya mabano mraba. Nafasi ya kwanza unaandika jina la makala inayoelekezwa na nafasi ya pili nyuma ya kigawanyishi unaandika maneno jinsi yanavyofaa katika sentensi yako.

Mfano: [[Kurasa uliyoilenga|maandishi yanayoonekana]] = maandishi yanayoonekana

Pia unaweza kutengeneza kiungo kuelekea sehemu mahususi ya makala kama kuna vichwa vya ndani ya makala:

[[Makala unapolenga#Sehemu ya makala yenye kichwa kidogo|maandishi yanayoonekana]] = maandishi yanayoonekana

Kiungo kuonekana kama italiki au koze

Iwapo unataka "maandishi yanayoonekana" ya kiungo kuonekana kama "italiki" weka apostrofi mbili kabla na baada ya mabano mraba kama hivi:

''[[Mapinduzi ya Viwandani]]'' = Mapinduzi ya Viwandani

(ukizoea utaangaza sehemu ya mabano mraba na kubofya alama ya " I " kwenye menyu ya kuhariri. Vilevile kwa kiungo kuonekana kama koze).

Kuhakikisha viungo ni sahihi

Tafadhali tazama viungo vyako ili kuhakikisha kwamba zimeelekezwa katika makala sahihi. Kwa mfano, Gibraltar imelengwa katika makala inayohusu eneo dogo la Kiingereza ndani ya Hispani, wakati Mlango wa Gibraltar ni jina la makala inayohusu mlango wa bahari kati ya Ulaya na Afrika karibu na Gibraltar.

Pia kuna kurasa za kutofautisha "maana" -- hizi siyo makala, bali kurasa zenye viungo vya makala zenye majina ya karibu. Tazama Kipanga (maana) kwa maana 4 tofauti.

Wakati wa kuunga

Kuongeza viungo kwenye makala inaleta maana zaidi, lakini viungo vingi zaidi huleta vurugu. Utaratibu ni fanya neno fulani mara moja tu kuwa kiungo katika makala moja usirudie neno hili kama kiungo. Unapaswa kuchagua mara ya kwanza ambako neno hiuli linatokeo kwenye makala.

Kuchungulia kwenye viungo vingine vya makala za Wikipedia pia inaweza kukusaidia kujifunza wakati kuweka viungo. Tazama ukurasa wa makala nzuri kwa orodha ya makala zenye ubora mkubwa sana.

Jamii au Category

Kila makala inatakiwa kuungwa katika jamii na makala nyingine zinazojadiliana mada za karibu.

Andika [[Jamii:]], na weka jina la jamii nyuma ya "nukta pacha" baina ya mabano ya miraba miwili.

Ni muhimu sana kuweka jamii sahihi kwa hiyo itakuwa rahisi kwa watu wengine kupata kazi yako. Njia iliyobora kutafuta jamii gani inayotakiwa iwekwe kwenye makala ni kuchungulia kurasa zenye kuelezea suala moja, na tazama jamii gani walizotumia.

Mfano: Unaandika makala kuhusu mnyama fulani. Chungulia kwa kuandika "jamii:wanyama" katika dirisha la "tafuta" na angalia vijamii vidogo vilivyopo tayari na makala zilizo ndani ya vijamii hivi.
Kwa habari zaidi, rejea katika ukurasa wa Jamii.
Jaribu ulichojifunza katika sanduku la mchanga

Endelea mwongozo na Kutaja vyanzo