Wikipedia:Makala ya wiki/Wolfgang Amadeus Mozart
Mandhari
Wolfgang Amadeus Mozart alikuwa mtunzi mashuhuri wa opera na mpigaji wa ajabu sana wa piano kutoka nchini Austria alipolizaliwa katika jiji la Salzburg tarehe 27 Januari 1756. Enzi za maisha yake mafupi, aliandika zaidi ya tungo 600 za muziki. Watu wanaamini kwamba huyu ni moja kati ya watunzi bora wa muda wote. Alitunga nyimbo kadhaa zikiwemo opera (muziki wenye hadithi) Don Giovanni na Die Zauberflöte (Filimbi ya Ajabu).
Kazi zake alizianza na minuet (dansi) aliyoitunga akiwa na umri wa miaka minne, na alizimalizia kwa kipande chake cha mwisho, Requiem, ambacho alikiacha hajakimaliza.
Mozart alikuja kufariki tarehe 5 Desemba 1791, akiwa na umri wa miaka 35. ►Soma zaidi