Nenda kwa yaliyomo

Watoto wanajeshi nchini Somalia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Watoto wanajeshi nchini Somalia ni suala kubwa ambalo linaendelea hata leo. Katika nchi ya Somalia, kumekuwa na vita vingi na migogoro mingi ambayo watoto wanajeshi wametumika. Katika vita vingi ambavyo vinajulikana kama "Vita vya Mogadishu", vikundi vyote ambavyo vilihusika katika vita hivyo vilitumia watoto kama wanajeshi. Baadhi ya vikundi hivyo ni: “Umoja wa Mahakama za Kiislamu”, “Muungano wa Marejesho ya Amani na Mapambano Dhidi ya Ugaidi”, na vikosi vya usalama vya “Serikali ya Mpito ya Shirikisho”.

Kikundi hicho cha mwisho kimeorodheshwa na Umoja wa Mataifa kuwa moja ya vikundi vikubwa ambavyo vinawaajiri na vinawatumia watoto katika jeshi na vikosi vyao vya usalama. Inafaa kukumbuka kuwa Umoja wa Ulaya na nchi ya Marekani kwa sasa ni wasaidizi wakuu wa vikosi vya usalama vya “Serikali ya Mpito ya Shirikisho” katika nchi ya Somalia. Tena nchi ya Marekani imelipa mishahara kwa vikosi vya usalama vya “Serikali ya Mpito ya Shirikisho”. Hii ina maana kwamba Marekani ni msaidizi mkubwa wa serikali ambayo inakiuka "Sheria ya Kuzuia Wanajeshi Watoto".

Pia, kikundi cha kigaidi ambacho kinajulikana kama al-Shabaab, ambacho kwa sasa kinapigana katika nchi ya Somalia ili kuanzisha Taifa la Kiislamu, ni kikundi kingine ambacho kinawaajiri na kinawatumia watoto kama wanajeshi katika vita vyao.

Jitihada za Jumuiya ya Kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

Katika mwaka wa 2017, Katibu Mkuu wa UM António Guterres alitoa maoni yake kuhusu ripoti kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Katika ripoti hiyo, ilionyeshwa kwamba kikundi cha kigaidi ambacho kinajulikana kama al-Shabaab, hutegemea sana wanajeshi watoto. Katika ripoti hiyo ilionyeshwa kwamba zaidi ya asilimia hamsini ya nguvu ya mapigano ya al-Shabaab inajumuisha wanajeshi watoto. Pia katika ripoti hiyo, ilionyeshwa kwamba katika al-Shabaab, kuna wanajeshi watoto wengi ambao wana umri wa miaka tisa tu ambao wanapelekwa kwenye mstari wa mbele katika vita na migogoro mingi.

Ripoti hiyo ilithibitisha kwamba watoto 6,163 waliajiriwa na walitumiwa katika vita na migogoro mingi kati ya tarehe 1 Aprili 2010 na 31 Julai 2016. Kati ya watoto hao, 230 walikuwa wasichana. Kati ya watoto hao wote, al-Shabaab waliajiri watoto 4,213 - asilimia sabini ya kesi ambazo zimethibitishwa. Pia, Jeshi la Kitaifa la Somalia liliajiri watoto 920 kati ya watoto hao.

Kabla ya ripoti hiyo, katika mwaka wa 2010, shirika lisilo la kiserikali kubwa ambalo linajulikana na "Human Rights Watch" kwa Kiingereza liliripoti kwamba kikundi cha kigaidi cha al-Shabaab kilikuwa kikiajiri watoto ambao wana umri wa miaka kumi tu ili kupigana katika vita na migogoro yao. Watoto hutekwa nyumbani na shuleni kwao, na mara nyingi darasa zima la watoto hutekwa ili kutumiwa kama wanajeshi katika vita na migogoro.

Katika mwaka 2012, Michelle Kagari, ambaye ni kiongozi msaidizi wa shirika lisilo la kiserikali kubwa lingine ambalo linajulikana kama “Amnesty International” kwa Kiingereza lilisema kwamba, ”Somalia si tu mgogoro wa binadamu: ni mgogoro wa haki za binadamu na mgogoro wa haki za watoto. Watoto wa Somalia hukabiliwa na hatari ya kifo kila wakati: kwa mfano, inawezekana kwamba watoto hao watauawa, kuajiriwa au kupelekwa kwenye mstari wa mbele. Inawezekana kwamba wao wataadhibiwa na al-Shabaab kwa sababu wanasikiliza muziki, au 'wamevaa nguo mbaya'. Pia, mara nyingi wao wanalazimishwa kujitunza peke yao kwa sababu wamepoteza wazazi wao. Pia, watoto wengi hupoteza uhai wao kwa sababu hawapati huduma ya matibabu ya kutosha.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Watoto wanajeshi nchini Somalia kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.