António Guterres
Mandhari
Antonio Manuel de Oliveira Guterres (alizaliwa 30 Aprili 1949) ni mwanasiasa wa Ureno ambaye anatumikia kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa tangu mwaka 2017. Hapo awali, alikuwa Kamishna wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) kati ya 2005 na 2015.
Guterres alikuwa Waziri Mkuu wa Ureno kutoka 1995 hadi 2002 na alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Kisoshalistu cha Ureano kutoka 1992 hadi 2002. Alihudumu kama Rais wa Umoja wa Vyama vya Kisoshalisti Duniani kutoka 1999 hadi 2005.
Katika kura ya kupima mawazo kwenye miaka 2012 na 2014 wananchi wengi wa Ureno walimtaja mara mbili alikuwa waziri mkuu bora wa nchi hii anayekumbukwa.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Wikimedia Commons ina media kuhusu: