Wamersedari wafiadini wa Damieta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Wamersedari wafiadini wa Damieta walikuwa walei watatu wa utawa wa Wamersedari waliokwenda Mashariki ya Kati kukomboa watumwa wakati wa vita vya msalaba (karne ya 13).

Tauni ilipoenea jeshini, walijitosa kuhudumia waliopatwa nayo.

Mwishoni walikamatwa na Waislamu na, kisha kuteswa sana, walitupwa chini kutoka mnarani huko Damieta (Misri).

Mfalme Ludoviko IX aliyekuweko vitani aliwasifu sana katika barua aliyomuandikia mwanzilishi wao, Petro Nolasko (1254).

Sikukuu ya hao watakatifu wafiadini huadhimishwa shirikani tarehe 11 Juni.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wamersedari wafiadini wa Damieta kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.