Wafiadini wa Amorio
Mandhari
Wafiadini wa Amorio (waliofariki 6 Machi 845 hivi) ni Wakristo 42 wenye vyeo au wa koo bora za mji huo wa Frigia, leo nchini Uturuki, waliofia dini yao kwa kuuawa na Waislamu waliowateka walipouvamia mwaka 838 chini ya Khalifa al-Mutasim. Kwa miaka yote saba walikataa kusilimu na hatimaye waliuawa kwenye mto Eufrate.
Kati yao wanajulikana kwa jina: Konstantino Baboutzikos, Theodoro Krateros, Esyo, Theofilo, Basoes, Kalisto na Konstantino mwingine[1].
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe ya kifodini chao.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Habari zao zilivyoandikwa na mmonaki Euodios muda mfupi baada ya kufia dini
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- (Kiingereza) Clive Foss (1991). "Amorion". In Aleksandr Petrovič Každan (ed.). The Oxford Dictionary of Byzantium. Oxford and New York: Oxford University Press. pp. 79–80. ISBN 0-19-504652-8.
- (Kiingereza) Aleksandr Petrovič Každan; Nancy Patterson Ševčenko (1991). "Forty-Two Martyrs of Amorion". In Aleksandr Petrovič Každan (a cura di). The Oxford Dictionary of Byzantium. Oxford and New York: Oxford University Press. pp. 800–801. ISBN 0-19-504652-8.
- (Kijerumani) Ralph-Johannes Lilie; Claudia Ludwig; Thomas Pratsch; Beate Zielke (2013). Prosopographie der mittelbyzantinischen Zeit Online. Berlin-Brandenburgische Akademie der Wissenschaften. Nach Vorarbeiten F. Winkelmanns erstellt. Berlin and Boston: De Gruyter.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |