Waanzilishi saba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mtakatifu Aleksi Falconieri.

Waanzilishi saba wa Utawa wa Watumishi wa Maria, ni wanaume wa Firenze (Italia) ambao mwaka 1233 hivi waliacha shughuli zao wakaenda kuishi upwekeni ili kuanzisha shirika la maisha ya wakfu aina ya ombaomba kwa heshima ya Bikira Maria.

Majina yao ni: Buonfiglio dei Monaldi (Bonfilius), Giovanni di Buonagiunta (Bonajuncta), Amadeus degli Amidei (Bartolomeus), Ricovero dei Lippi-Ugguccioni (Ugo), Benedetto dell'Antella (Manettus), Gherardino di Sostegno (Sostene), na Alessio de' Falconieri (Alexius), wa mwisho kufa (1310), ambaye ndiye maarufu zaidi.

Wote wanaheshimiwa katika Kanisa Katoliki kama watakatifu, na sikukuu yao ya pamoja huwa tarehe 17 Februari.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]