Viktorini wa Camerino
Mandhari
Viktorini wa Camerino (Settempeda, leo San Severino Marche, Italia 470 hivi - Pioraco, 538) alikuwa Mkristo ambaye, alipofiwa wazazi wake, aliamua pamoja na ndugu yake Severino wa Settempeda kuwagawia maskini urithi wao mkubwa na kwenda kuishi upwekeni kwenye Mlima Nero.
Papa Vigili alimfanya yeye askofu wa Camerino (Italia ya Kati) na Severino askofu wa Settempeda[1].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |