Nenda kwa yaliyomo

Vanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Vanga (jenasi))
Vanga
Vanga kichwa-cheupe
Vanga kichwa-cheupe
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Corvoidea (Ndege kama kunguru)
Familia: Vangidae (Ndege walio na mnasaba na vanga)
Ngazi za chini

Jenasi 15:

Vanga (kutoka Kimalagasi: vanga) ni ndege wa familia Vangidae. Wanatokea Madagaska tu isipokuwa vanga buluu wa Komori ambaye anatokea kisiwa cha Mwali katika Komori. Takriban spishi zote zina rangi ya nyeusi, kijivu au kahawa juu na nyeupe au pinki chini, lakini chache zina rangi ya buluu na vanga domo-buluu ni mweusi mwenye mgongo mwekundu na vanga wa Bernier ni mweusi kabisa (jike ana rangi ya kahawa). Ndege hawa wana sauti ya filimbi. Hula wadudu, nyungunyungu, mijusi na amfibia, pengine matunda pia. Hulijenga tago lao kwa vijiti, chamba cha mti, mizizi na majani mtini. Jike huyataga mayai 2-4.

Makala hii kuhusu "Vanga" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili vanga kutoka lugha ya Kimalagasi. Neno (au maneno) la jaribio ni vanga.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.