Uwanja wa michezo wa Kadinali Malula

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa Kadinali Malula wakati wa ukoloni ulipoitwa kwa heshima ya malkia Astrid

Uwanja wa michezo wa Kadinali Malula (awali ulikuwa ukijulikana kama Stade 24 Novembre ) ni uwanja wa michezo uliopo Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ulifunguliwa mnamo mwaka 1937 na unatumika kama uwanja wa nyumbani wa timu ya AS Dragons.

Hivi sasa umeitwa kwa jina la heshima la Joseph Malula ambaye alikua Askofu Mkuu wa Kinshasa kutoka mwaka 1964 hadi kifo chake mnamo mwaka 1989. Alikuwa kadinali wa Kanisa Katoliki tangu mwaka 1969.

Uwanja huu wa Kadinali Malula ulitajwa hapo awali, tarehe ambayo Mobutu Sese Seko alichukua mamlaka nchini Kongo mnamo mwaka 1965. Hapo awali ulipewa jina la Astrid wa Uswidi, Malkia wa Wabelgiji, wakati huo Kongo ilikuwa chini ya koloni la Mbelgiji.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Kadinali Malula kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.