Utumbo mwembamba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Utumbo mwembamba ni sehemu ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula iliopo kati ya tumbo na utumbo mpana. Ni sehemu ndefu ya mfumo huo yenye urefu wa mita 4.5 - 9.6 kwa mtu mzima. Ndiyo sehemu ambapo virutubishi vingi hufyonzwa na kuingizwa katika mfumo wa damu ili kusambazwa sehemu mbalimbali za mwili.

Sehemu kubwa ya mmeng'enyo wa chakula inatokea hapa, yaani ni katika sehemu hii kwamba mwili unatoa virutubishi vyake kutoka ujiuji wa chakula kilichotafunwa mdomoni na kupasuliwa kikemia tumboni.

Utumbo mwembamba huwa na sehemu tatu

Inapokea kiowevu cha nyongo na cha kongosho kwa njia ya kipito cha nyongo. Upande wa ndani wa utumbo huwa na mikunjo mingi pamoja na vili ambayo ni vimbe kama vidole vidogo vyote vinayoongeza eneo linalopatikana kwa mmeng'enyo wa chakula.

Ujiuji wa chakula unatoka kwenye tumbo na kuingia katika sehemu ya duodeno lenye urefu wa sentimita 24. Hapa kiwango cha asidi katika tope la chakula kinapunguzwa.

Katika jejuno kiowevu cha kongosho kinapasua wanga, protini na mafuta kwa sehemu zinazoweza kupokewa na damu. Kiowevu cha nyongo kinasaidia upasuaji wa mafuta. Molekuli zinazopatikana baada ya hatua hiyo zinapita katika ngozi ya utumbo na kupelekwa katika ini ambako zinashughulikiwa tena. Utumbo mwembamba unapokea pia sehemu kubwa ya maji yanayohitajika mwilini na kuiondoa katika tope la chakula.

Katika sehemu ya ileo ni hasa vitamini zinazopokewa na kupitishwa kwenda damu.

Kutoka hapo mabaki ya chakula yanaendelea katika utumbo mpana.

Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Utumbo mwembamba kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.