Nenda kwa yaliyomo

Usawa wa kijinsia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Usawa wa Kijinsia)
Ishara ya usawa wa kijinsia.

Usawa wa kijinsia ni lengo la jitihada za kuleta usawa kati ya jinsia zote mbili na kuondokana na dhuluma mbalimbali za jinsia moja dhidi ya nyingine zilizotawala historia ya binadamu.

Usawa wa kijinsia unahusiana na haki za binadamu, hasa haki za wanawake na maendeleo ya kiuchumi. UNICEF inafafanua usawa wa kijinsia kama "kusawazisha uwanja wa kucheza kwa wasichana na wanawake kwa kuhakikisha kwamba watoto wote wana fursa sawa ya kuendeleza vipaji vyao".

Mfuko wa Idadi ya Watu wa Umoja wa Mataifa (United Nations Population Fund) ulitangaza usawa wa kijinsia "kwanza kabisa kama haki ya binadamu".

Usawa wa kijinsia ni mojawapo kati ya malengo ya "mradi wa Milenia" wa Umoja wa Mataifa unaotarajia kumaliza umaskini ulimwenguni ufikapo mwaka 2015; mradi huo unadai, "Kila lengo linahusiana moja kwa moja na haki za wanawake, na jamii ambamo wanawake hawana haki kama za wanaume kamwe haziwezi kufanikisha maendeleo kwa namna endelevu".

Hivyo, kukuza usawa wa kijinsia kunaonekana kama himizo kwa mafanikio makubwa ya uchumi. Kwa mfano, mataifa ya Kiarabu ambayo yanawanyima wanawake usawa yalionywa katika ripoti iliyofadhiliwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2008 kwamba kitendo cha kuwanyima mamlaka wanawake ni kipengele muhimu kinachodhalilisha kurudi kwa mataifa hayo katika nafasi ya kwanza ya uongozi wa dunia katika biashara, elimu na utamaduni.

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje