Upangaji wa harusi
Mandhari
Harusi ni sherehe ya maana sana katika maisha ya binadamu.
Siku ya harusi ni kubwa sana kwa bwana na bibi harusi ambapo wanauacha ukapera na kuingia katika ushirika mwingine ambapo watakuwa kitu kimoja.
Harusi ni ya maana sana katika jamii za Afrika ambapo kijana akifikia kuoa huonekana kama mtu mkubwa atakayeweza sana kufanya maamuzi kwa familia yake.
Mwanamke pia huwa na uchu wa kuolewa ili aweze kupata familia yake, kulea watoto na pia kuangalia mumewe.
Mipango ya harusi
[hariri | hariri chanzo]Kabla ya siku hii kubwa ya harusi, mipango kabambe hufanywa ili kila kitu kiwe shwari.
Katika jamii nyingi, watu hualikwa ili waweze kuwashuhudia bibi na bwana harusi wakifunga ndoa.
Harusi huenda ikafanyika kwenye kanisa au mskiti, na hata kwa mkuu wa wilaya hiyo.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Upangaji wa harusi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |