Ununbi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search


Ununbi (Ununbium)
Uub-TableImage.png
Jina la Elementi Ununbi (Ununbium)
Alama Uub
Namba atomia 112
Mfululizo safu matali za mpito (?)
Uzani atomia 277 g/cm³ (kadirio)
Valensi 2, 8, 18, 32, 32, 18, 2
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Asilimia za ganda la dunia 0% (elementi sintetiki)
Hali maada huaminiwa kuwa gesi au kama metali
Mengineyo Ununubi ni elementi sintetiki yenye nusumaisha mafupi sana iliyotengenezwa mara nne tu

Ununbi ni elementi sintetiki yenye namba atomia 112 kwenye mfumo radidia, uzani atomia ni takriban 277. Alama yake ni Uub. Si rahisi kutaja tabia zake kwa sababu imetengenezwa mara nne tu katika maabara kama atomi moja-moja.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Jina latokana na maneno ya kilatini kwa "1" (unum) na kwa "2" (bi). Un-un-bi yamaanisha hivyo moja-moja-mbili yaani namba atomia ya elementi. Ununbi ni jina la muda inawezekana ya kwamba jina lingine litatolewa kama wataaalamu hukubaliana.

Ufumbuzi[hariri | hariri chanzo]

Elementi iliwahi kutabiriwa na wanasayansi kuwa inaweza kupatikana. Ilitengenezwa mara ya kwanza 1996 na wanasayansi wa taasisi ya utafiti wa kinyuklia huko Darmstadt kwa kufyatulia viini vya atomi za zinki katika risasi.

Matumizi[hariri | hariri chanzo]

Kama elementi zote za sintetiki haina matumizi bado zatengenezwa tu kwa kusudi la utafiti. Duniani hazipatikani kiasili tena. Kuna uwezekano ya kwamba ziliwahi kupatikana zamani ila tu kutokana na maisha mafupi ya atomi zao zimeshapotea muda mrefu.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: