Tumati
Tumati ni kata ya Wilaya ya Mbulu katika Mkoa wa Manyara, Tanzania. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,798 waishio humo.[1]
Kata ya Tumati inajumuisha vijiji vya Tumati, Mongahay, Endoji, Endesh na Getesh. Kata hii ni miongoni mwa kata zilizoongoza Tanzania kuwa na shule nyingi za wananchi za kata. Kabla ya kata kugawanywa mwaka 2009 ilkuwa na shule 3 za sekondari za wananchi shule hizo ni Tumati, Yaeda Ampa na Endoji. Kwa sasa zipo shule 2 za Tumati na Endoji baada ya shule ya Yaeda Ampa kuwa katika kata mpya ya Yaeda Ampa. Zipo shule 7 za msingi ambazo ni Tumati, Mongahay, Yerotamburda, Endesh, Endoji, Erboshan na Getesh.
Kata hii ipo katika uwanda wa juu na inapakana na msitu mnene wa Nowu kwa upande wa mashariki, kaskazini kata ya Yaeda Ampa, magharibi kata ya Dongobesh na kusini wilaya ya Babati. Eneo kubwa la kata hii lina baridi kali kwa mwaka mzima, hasa vijiji vya Tumati, Mongahay na Endesh.
Shughuli za kilimo ndio shughuli kubwa katika kata hii; mazao yalimwayo ni mahindi, maharage, viazi mviringo na vitunguu saumu ambapo wenyeji wanayaita mashamba ya zao hili kuwa ni "migodi" au "myumba za kupanga" kutokana na fedha nyingi zinazotokana na zao hilo.
Wenyeji wa kata hii ni wa kabila la Wairaqw kwa zaidi ya asilimia 98. Mbali na kilimo wenyeji pia wanajishughulisha na ufugaji.
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
![]() |
Kata za Wilaya ya Mbulu - Mkoa wa Manyara - Tanzania | ![]() |
---|---|---|
Ayamaami | Ayamohe | Bargish | Bashay | Daudi | Dinamu | Dongobesh | Endagikot | Endamilay | Eshkesh | Gehandu | Geterer | Gidihim | Gunyoda | Hayderer | Haydom | Imboru | Kainam | Maghang | Marang | Maretadu | Masieda | Masqaroda | Murray (Mbulu) | Nahasey | Nambisi | Sanu Baray | Tlawi | Tumati | Uhuru | Yaeda Ampa | Yaeda Chini |
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Manyara bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Tumati kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
|