Troia
Troia (kwa Kigiriki: Τροία, troia, pia: Ίλιον, ilion; kwa Kiingereza: Troy)[1] ulikuwa mji wa Asia Ndogo zamani za Ugiriki ya Kale. Inajulikana kutokana na utenzi wa Iliadi ambamo mshairi Homer alisimulia habari za Vita ya Troia.[2]
Kwa karne nyingi mahali pa mji hapakujulikana ingawa watu wengi walijaribu kupakuta kwa sababu ya umaarufu wa utenzi huo uliokuwa na maana sana katika utamaduni wa Ulaya. Mnamo mwaka 1868 Mjerumani Heinrich Schliemann alianza kuchimba kwenye kilima cha Hisarlik kilichopo karibu na mji wa Çanakkale magharibi kaskazini mwa Uturuki. Alikuta mabaki ya majengo na kuta kubwa na baada ya majadiliano marefu leo hii wataalamu hukubaliana hapa palikuwa mahali pa Troia ya Kale.
Maghofu ya Troia yamepokelewa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO. Azimio hili lilitolewa kwa maelezo yafuatayo:
"Mahali pa kiakiolojia pa Troia ni muhimu sana kwa kuelewa vyanzo vya maendeleo ya ustaarabu wa Ulaya. Pana pia umuhimu mkubwa wa kiutamaduni kutokana na athira kubwa ya Iliadi ya Homer juu ya sanaa kwa muda wa zaidi ya milenia mbili". [3]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Lewis, Charlton T. "Ilium". A Latin Dictionary. Tufts University: The Perseus Digital Library. Iliwekwa mnamo 2008.
{{cite web}}
: Check date values in:|accessdate=
(help); Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help) - ↑ March, Jenny (2008). The Penguin Book of Classical Myths. Penguin Books. uk. 294. ISBN 978-0-141-02077-8.
- ↑ UNESCO citation
Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Troia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |