Thoma wa Celano
Thoma wa Celano (kwa Kiitalia Tommaso da Celano; 1200 hivi – 1265 hivi) alikuwa mfuasi wa Fransisko wa Asizi katika utawa wa Ndugu Wadogo, mshairi, na mwandishi wa vitabu vitatu rasmi juu ya mwanzilishi huyo.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Thoma alikuwa mwenyeji wa Celano (leo katika mkoa wa Abruzzo (Italia).
Thoma hakuwa kati ya wafuasi wa kwanza kabisa wa Fransisko, lakini alijiunga naye mwaka 1215 hivi.
Mwaka 1221 alitumwa naye Ujerumani ili kuanzisha shirika huko, na mwaka 1223 akawa mkuu wa kanda ya Rhineland, yenye konventi za Cologne, Mainz, Worms na Speyer.
Baada ya miaka michache alirudi Italia, alipobaki mpaka mwisho wa maisha yake.
Mwaka 1260 alihamia Tagliacozzo ili kushughulikia Waklara wa huko, na ndipo alipofariki kati ya mwaka 1260 na 1270.
Maandishi
[hariri | hariri chanzo]Kitabu cha kwanza aliagizwa na Papa Gregori IX mwaka 1228 wakati wa kumtangaza Fransisko kuwa mtakatifu. Cha pili aliagizwa na Kreshensi wa Iesi, mkuu wa shirika kati ya miaka 1244 na 1247. Cha tatu kinahusu miujiza ya Fransisko na kiliagizwa na mkuu mpya wa shirika Yohane wa Parma kati ya 1254 na 1257.
Thoma aliandika pia tenzi Fregit victor virtualis na Sanctitatis nova signa kwa heshima ya Fransisko.
Pengine aliandika pia Maisha ya Mt. Klara wa Asizi, na utenzi "Dies Irae".
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Thoma Archived 7 Aprili 2005 at the Wayback Machine. (katika tovuti rasmi wa kijiji cha Celano)
- Vitabu vitatu vya Thoma wa Celano kuhusu Fransisko wa Asizi Archived 23 Machi 2005 at the Wayback Machine. (kwenye Franciscan Cyberspot)
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |